SYRIA-IS-PALMYRA-UHARIBIFU-USALAMA

Kundi la IS laishambulia hekalu maarufu ya Palmyra

Mji wa kale wa Palmyra (mwaka 2010).
Mji wa kale wa Palmyra (mwaka 2010). REUTERS/Mohamed Azakir

Wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Islamic State (IS) wameteketeza Hekalu ya Baalshamin katika mji wa kale wa Palmyra, amesema Jumapili mkurugenzi wa Mambo ya Kale nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

" Daech [neno la Kiarabu linalotafsiri kwa kifupi IS] kwa siku ya leo imeweka kiasi kikubwa cha vilipuzi katika Hekalu ya Baalshamin kabla kulipuka. Jengo hilo kwa kiasi kikubwa limeharibiwa. Cella [sehemu inayofungwa ya hekalu] imeteketezwa na nguzo zilikua pembezoni zimeporomoka ", amesema Maamoun Abdulkarim.

Hekalu ya Baalshamin ilianza kujengwa katika mwaka wa 17 na ilikarabatiwa na Mfalme wa Kirumi Hadrian, katika mwaka wa 130. Baalshamin ni mungu wa Kifinisia.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State " waliwanyonga watu kadhaa katika mji wa kale wa Palmyra. Mwezi Julai waliharibu sanamu maarufu la Simba wa Athena, ambayo ilikuwa katika mlango wa jumba la Makumbusho la Palmyra, na Jumba hilo lilibadilishwa kuwa mahakama na jela. wapiganaji hao pia walimuuawa Jumanne wiki iliopita mkurugenzi wa Mambo ya Kale wa mji wa Palmyra, Khaled al-Assad ", amesema Maamoun Abdulkarim.

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria (OSDH) limehibitisha uharibifu wa mnara huo wa kihistoria. Mwishoni mwa mwezi Mei, wapiganaji wa kundi la Islamic State waliuchukua kutoka mikononi mwa jeshi la Syria mji wa Palmyra na kitongoji chake cha kale maarufu duniani kilochotangazwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.