SYRIA-IS-MAPIGANO-MAUAJI-USALAMA

Syria: watu 26 wauawa katika mashambulizi 2 yanayodaiwa kuendeshwa na IS

Raia wa Syria wanakagua eneobaada ya shambulio katika mji wa Hasaka, kaskazini mashariki mwa Syria, Agosti 19, 2015.
Raia wa Syria wanakagua eneobaada ya shambulio katika mji wa Hasaka, kaskazini mashariki mwa Syria, Agosti 19, 2015. AFP/AFP/Archives

Watu 26 wameuawa Jumatatu wiki hii katika mashambulio mawili ya mabomu yaliyotegwa katika gari ndogo katika mji wa Hasaka nchini Syria. Mashambulizi ambayo yamedaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State, shirika lisilo la kiserikali limebaini.

Matangazo ya kibiashara

Milipuko hiyo imewaua raia 13 wa kawaida, ikiwa ni pamoja na watoto wawili, maafisa sita wa usalama kutoa jamii ya Wakurdi na wapiganaji saba wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali katika mji ulio kaskazini mashariki ya nchiya kunakoshuhudiwa mapigano, Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limebaini.

Kundi la Islamic State tayari limelenga mara kadhaa mji wa Hasaka namkoa wake, ambapo wanamgambo wa Kikurdi na vikosi vinavyomuunga Rais Bashar al-Assad wanachangia udhibiti.

Kwa mujibu wa OSDH, bomu lililotegwa katika gari ndogo ililipuka katika eneo la ukaguzi la Wakurdi katika kitongoji cha Khashman, na kuwaua rwatu10 na wapiganaji sita wa Kikurdi. Shambulio la pili, limetokea katika wilaya ya al-Mahata, na inaonekana limelenga makao makuu ya Jeshi la Taifa (wanaoiunga mkono serikali) na kuwaua askari saba wa kitengo hiki na watu watatu. Karibu watu 80 wamejeruhiwa.

Kundi la Islamic State limekiri kuhusika na mashambulizi hayo mawili