URUSI-MAREKANI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Obama akutana na Putin kwenye UN, lakini watafautiana kuhusu Syria

Marais wa Urusi Vladimir Putin na Marekani, Barack Obama, Septemba 28, 2015 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Marais wa Urusi Vladimir Putin na Marekani, Barack Obama, Septemba 28, 2015 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. érôme CARTILLIER et Max DELANY | AFP

Barack Obama na Vladimir Putin walikutana Jumatatu wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika kutafuta ufumbuzi wa machafuko nchini Syria, bila hata hivyo kuafikiana, hasa juu ya hatma ya Bashar Al Assad.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo uliyodumu dakika 90, ambao ulianza katika hali ya furaha, Rais wa Urusi alizungumzia mkutano wenye lengo la " kujenga na kudumisha ushirikiano " na mwenzake wa Marekani na amesema uwezekano wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Hata hivyo Rais Putin ameonyesha tofauti halisi juu ya jinsi ya kumaliza vita ambavyo tayari vimewaua zaidi ya watu 240,000

Putin hakuweka kando mashambulizi ya Urusi, lakini ametupilia mbali madai ya kutumwa kwa wanajeshi Urusi nchini Syria kwa lengo la kupambana dhidi ya wanajihadi wenye msimamo mkali wa kundi la Islamic State(IS), na kuweka mbele nia yake ya kusaidia jeshi la Syria katika vita hivyo dhidi ya IS.

Ushahidi wa mvutano unaoendelea na nchi za Magharibi, kiongozi wa Kremlin amepinga majaribu ya Barack Obama na Francois Hollande: " Ninawaheshimu marais wenzangu wa Marekani na Ufaransa lakini wao si raia wa Syria na kwa hiyo hawapaswi kujihusisha katika kuwachagua viongozi wa nchi nyingine ".

Mkutano huu wa kwanza kati ya Obama na Putin tangu zaidi ya miaka miwili iliyopita uligubikwa na masuala mawili, ikiwa ni pamoja na hali inayoendelea Syria pamoja na machafuko yanayoendelea mashariki mwa Ukraine.

Hata hivyo Marais wa Marekani na Ufaransa wamesema Rais wa nchi Syria Bashar Al Assad anatakiwa kuachia ngazi ili machafuko nchini humo yapatiwe ufumbuzi.