UN-PALESTINA-DIPLOMASIA

Bendera ya Palestina yapandishwa kwenye Umoja wa Mataifa

Bendera ya Palestina ikipandishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 30, 2015
Bendera ya Palestina ikipandishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 30, 2015 AFP/AFP

Jumatano hii, Septemba 30, bendera ya Palestina imepandishwa kawa mara ya kwanza mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Palestina iliteuliwa mwaka 2012 kuwa mwangalizi katika Umoja wa Mataifa, lakini ilichukua hadi katikati mwa mwezi Septemba ili kuruhusu bendera yake kuelea mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Bendera hii ya Palesyina yenye rangi nyekundu, nyeusi, nyeupe na kijani imepandishwa saa 7:15 (sawana saa 11:15 jioni saa za kimataifa) katika bustani ya taasisi ya kimataifa, na toka leo Jumatano itakua sambamba na bendera193 za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Vatican, ambayo, kama Palestina, inatambuliwa kama taifa lisilokuwa mwanachama.

" Katika wakati huu wa kihistoria, ninawaambia watu wangu kila mahali pandisha juu kabisa bendera ya Palestina, kwa sababu ni ishara ya utambulisho wetu. Hii ni siku ya kujisifu ", amesema Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, mapema katika sherehe iliyohudhuriwa na mamia ya watu, ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Abbas, muda mfupi kabla alitangaza katika jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba Palestina inatakiwa kutambuliwa kama taifa huru linalojitegemea.

Huu ni ushindi wa kidiplomasia kwa mamlaka ya Palestina, lakini jambo hili linashutumiwa na wawakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa. Katika Majimbo Yanayokaliwa, wakati baadhi ya wanakaribisha hatua hii mpya kuelekea kutambuliwa kimataifa kwa taifa la Palestina, watu wengi wanajua kwambahali hii haitoleta mabadiliko katika maisha yao ya kila siku.

Vita nchini Syria, harakati za makundi ya kigaidi au mgogoro wa wahamiaji vinawatia wasiwasi viongozi na marais wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, sawa na hali inayoendelea katika majimbo ya Gaza na Cisjordania, amearifu mwandishi wetu nchini Marekani, Anne Corpet, ambaye amekumbusha kwamba sababu ya Palestina, kuwepo katika mkutano huo, kumepelekea iwekwe katika agenda ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Mwaka huu.

Kwa karibu miaka 70, suala la Palestina lilipelekea kuchukuliwa maazimio mengi katika Umoja wa Mataifa, ambapo ilipewa kipaumbele katika mijadala mbalimbali. Baadhi ya maazimio hayo licha ya kuwa ni machache yalitekelezwa, na miradi mingi ilijikuta ikikabiliwa na upinzani mkubwa wa kura ya turufu ya Marekani. Katika hotuba inayosubiriwa sana kwenye jukwa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumatano wiki hii, Rais wa Mamlaka ya Palestina atachukua nafasi hiyo kwa kuiomba jumuiya ya kimataifa kuchangia juu ya hatma ya watu wake.