AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban yatimuliwa Kunduz

Alhamisi wiki hii majeshi ya Afghanistan yameurejesha kwenye himaya yao mji wa Kunduz uliokua ukishikiliwa kwa muda wa siku tatu na wapiganaji wa kundi la Taliban.

Mwanajeshi wa Afghanistan aliyejeruhiwa katika mapigano na Taliban ahamishwa na kupelekwa na wenzake, Septemba 30, 2015.
Mwanajeshi wa Afghanistan aliyejeruhiwa katika mapigano na Taliban ahamishwa na kupelekwa na wenzake, Septemba 30, 2015. STR/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii, kwa kuwa ni muhimu, hata hivyo, ni mbali na kuashiria ushindi wa muda mrefu dhidi ya Taliban katika mji wa Kabul, kutokana na vita vya maguguni vinavyodumu tangu kuanguka kwa utawala wao karibu miaka 14 iliyopita.

Kuudhibiti mji wa Kunduz, ni ushindi mkubwa kwa utawala wa Ashraf Ghani, madarakani kwa mwaka mmoja sasa, na vikosi vya Afghanistan, ambavyo viko kwenye safa ya mbele tangu kumalizika kwa ujumbe wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) Desemba mwaka jana.

NATO kwa sasa ina wanajeshi 13,000 tu nchini Afghanistan, ambao majukumu yao ni kutoa ushauri na mafunzo. Lakini kutokana na vita vinavyolikabili jeshi la Afghanistan, wanajeshi wa Ujerumani, Marekani na Uingereza kutoka vikosi maalum walipelekwa katika Kunduz. Jeshi la Marekani pia liliendesha mashambulizi mengi ya anga kadhaa, ikiwa ni msaada mkubwa kwa jeshi la Afghanistan.

Tangu Alhamisi asubuhi wiki hii, vikosi maalum vya Afghanistan vinaudhibiti mji wa Kunduz, kwa mujibu wa Sediq Sediqqi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan, kwenye Twitter. naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ayoub Salangi amethibitisha kwamba mji wa Kunduz umedhibitiwa katika neema ya "operesheni maalum" wakati ambapo mapigano makali yamekua yakiendelea.

Kwa mujibu wa mkazi mmoja aliyewasiliana na shirika la habari la Ufaransa la AFP, vita vya hapa na pale vimekua vikiendelea Alhamisi asubuhi katika baadhi ya maeneo, na miili ya wapiganaji wa Taliban imetapakaa katika mitaa ya mji wa Kunduz.

Mji wa Kunduz una wakazi 30,000, ambao baada ya kutekwa na wapiganaji wa taliban , baadhi ya wakazi hao walikimbilia katika mikoa jirani.