Syria: watu wasiopungua 26 wauawa katika mashambulizi ya anga
Watu wasiopungua 26 wameuawa Jumatatu hii kaskazini mwa Syria katika mashambulizi ya anga yanayokisiwa kutekelezwa na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, shirika la Haki za Binadamu (OSDH) limetangaza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
atoto saba na wanawake wanne ni miongoni mwa watu waliouawa katika mashambulizi hayo yaliolenga kijiji cha Al-Hol, ambacho mwezi uliopita kiliondolewa mikononi mwa kundi la Islamic State (IS) na waasi wa Kiarabu na wa Kurdi, shirika la haki za binadamu limeeleza.
Mapema Jumatatu wiki hii serikali ya Syria imeunyooshea kidole cha lawama muungano wa kimataifa kuendesha mashambulizi kwa mara ya kwanza katika kambi ya jeshi kuuawa wanajeshi kadhaa, madai ambayo yamekanushwa na muungano unaoongozwa na Marekani, ambao umethibitisha kuwa mashambulizi yake yamelenga kundi la Islamic State (IS).
Damascus imejibu kwa nguvu baada ya vifo vya askari wake watatu waliouawa siku ya Jumapili katika mashambulizi ya angani katika kambi ya jeshi ya Deir Ezzor, mashariki mwa Syria.
Damascus imeushtumu moja kwa moja "muungano unaoongozwa na Marekani" kwa "uchokozi wa wazi" ambao "unakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa."
"Tunatoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua muhimu ili kuzuia tukio kama hili lisirudi si kutokea", wizara ya mambo ya nje imeongeza katika barua iliyomtumia Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja huo.
Alhamisi Desemba 4, Uingereza iliendesha mashambulizi yake ya kwanza ya anga nchini Syria dhidi ya ngome za kundi la Islamic State, masaa kadhaa tu baada ya kupewa idhni na Bunge.
Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye anaongoza muungano wa washirika nchini Syria dhid ya IS, alikaribisha uamzi huo, akisema kwamba Marekani imekua ikisubiri jeshi la anga la Uingereza kujiunga katika shughuli za kijeshi nchini Syria.