AFGHANISTAN-TALIBAN-IS-MAPIGANO

Zaidi ya watu 50 wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya Taliban

Mullah Omar, kiongozi mkuu wa Taliban, akizungukwa na askari wake, mwaka 1996.
Mullah Omar, kiongozi mkuu wa Taliban, akizungukwa na askari wake, mwaka 1996. AFP PHOTO / BBC TV / BBC NEWSNIGHT / FILES

Zaidi ya watu 50 wameuawa na wengine arobaini kujeruhiwa katika mapigano mapya kati ya makundi hasimu ya Taliban katika wilaya ya Shindand, karibu na mji wa Herat, magharibi mwa Afghanistan, polisi imesema Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya mwisho ya hivi karibuni yanaonyesha mgawanyiko mkubwa katika kundi la "Wanafunzi wa dini" tangu kuthibitishwa, mwezi Julai, kwa kifo cha mwanzilishi wao, Mullah Omar, mwaka 2013.

Baadhi ya makundi yakataa mamlaka ya mrithi wake, Mullah Akhtar Mansour, na kulazimisha kiongozi mpya ateuliwe. Mapigano ya mara kwa mara tayari yametokea kati ya makundi hasimu ya Taliban. Mapigano ambayo yamesababisha vifo kadhaa.

Kwa mujibu wa Ehsanullah Hayat, msemaji wa polisi katika mji wa Herat, wapiganaji 54 wameuawa na wengine arobaini kujeruhiwa katika mapigano kati ya wapiganaji wanaomtii Mullah Mansour na wafuasi wa mpinzani wake, Mullah Mohammad Rasool Akhund.

Mapigano haya mapya ni moja ya sababu za utatanishiwa siku nyingi kuhusu hatma ya Mullah Mansour. Taarifa kuhusu kujeruhiwa vibaya kwa Mullah Mansour katika urushianaji risasi na wapiganaji wengine wa Taliban zimekanushwa na mkanda wa sauti yake uliorekodiwa ambao unaonyesha kuwa bado yupo hai.

Hata hivyo, kuna video iliyorushwa hewani inayomuoyesha raia wa Afghanistan, ambaye ni mpiganaji wa kundi la Islamic State akilituhumu kundi la Taliban kufanya kazi chini ya ukaguzi wa Idara ya ujasusi ya Pakistan (ISI), kwa kutozingatia sheria za kiislamu na kujiunga na Iran yenye waumini wengi wa Kishia.

Ujumbe huu, uliyosainiwa na mwanaharakati aitwaye Yasir Abdu al Afghani, unaeleza uhasama mkubwa kati ya wafuasi wa kundi la Islamic State na Taliban.

"Ndugu zangu, pingamizi yetu kubwa kwa Uongozi wa kiislamu (Taliban) inahusu uhusiano wake na Pakistan pamoja na ushirikiano wake na ISI (...)", mwanaharakati huyo amesema katika video.