SYRIA-MAPIGANO-USALAMA

Syria: wanajeshi watiifu kwa serikali wakidhibiti kijiji muhimu

Askari waminifu kwa serikali ya Syria ya Bashar al-Assad Jumatano hii, wamekidhibiti tena kijiji muhimu katika mkoa wa pwani wa Latakia, inakoishi familiaya Assad, shirika la habari la serikali SANA limearifu.

Picha ya shirika la habari la Syria SANA la majengo katika mji wa Latakia nchini Syria, Novemba 10, 2015 baada ya shambulio.
Picha ya shirika la habari la Syria SANA la majengo katika mji wa Latakia nchini Syria, Novemba 10, 2015 baada ya shambulio. AFP/SANA/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Likinukuu chanzo cha kijeshi, shirika hilo limesema kwamba vikosi vya jeshi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali walikuwa "wamelidhibiti eneo lote muhimu la Jabal Nuba baada ya kuwaua magaidi kadhaa."

Vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Syria vikisaidiwa na ndege za kivita za Urusi wameongeza mashambulizi yao katika wiki za hivi karibuni katika eneo hilo.

Jumatano hii, wameendesha operesheni ya kijeshi katika "msitu mkubwa na katika eneo jingine baya" kabla ya kukagua eneo hilo, shirika la habari la serikali SANA limeongeza.

Jeshi limeendelea "kudhibiti" hali ya mambo karibu na ngome za waasi, ikiwa ni pamoja na kijiji cha Salma, ambacho kilikua kikidhibitiwa kwa zaidi ya miaka miwili na wapinzani wa utawala wa Assad na ambacho kimekukua kikilengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi. Urusi lianza kuingilia kati kijeshi nchini Syria tarehe 30 Septemba 2015 kwa kuendesha mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha yanayoipinga serikali, makundi ambayo ni yenye msimamo wa wastani kwa wanajihadi.

Shirika lisilo la kiserikali limethibitisha kuwa vikosi vya jeshi vikisaidiwao na kundi la Mashia wa Lebanon la Hezbollah walichukua udhibiti wa eneo la Jabal Nuba.