SYRIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Syria: watu zaidi ya 20 wauawa katika mashambulizi ya jeshi

Watu wasiopungua 20, wakiwemo watoto saba, wameuawa Alhamisi hii katika mashambulizi ya anga ya majeshi ya serikali ya Bashar al-Assad dhidi ya kijiji kimoja, kusini mwa mji wa Damascus, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limesema.

Idleb baada ya mji wa kaskazini magharibi mwa Syria kulengwa na mashambulizi, Desemba 20, 2015.
Idleb baada ya mji wa kaskazini magharibi mwa Syria kulengwa na mashambulizi, Desemba 20, 2015. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Watu wasiopungua kumi pia wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo katikati mwa kijiji cha Hammouriyé, kijiji cha eneo la mashariki, ngome kubwa ya waasi katika mkoa wa Damascus ambao hushambuliwa mara kwa mara na majeshi ya serikali, Mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdel Rahman amebaini.

Raia wawili pia wameuawa katika urushaji makombora dhidi ya mji wa Duma, kaskazini mashariki mwa mji wa Damascus, wakati ambapo eneo la mashariki limekua likilengwa na mashambulizi makali ya vikosi vya serikali, amesema Bw. Abdul Rahman.

Waasi mara nyingi hurusha makombora katika mji mkuu kutoka eneo la mashariki, mashariki mwa mji wa Damascus.

Kwa kipindi cha miaka mitano ya vita nchini Syria, watu zaidi ya 250,000 wameuawa na mamilioni wengine wamelazimika kuyahama makazi yao.