Askari polisi 12 wa Iraq wauawa katika shambulio la IS
Washambuliaji wa kujitoa mhanaga wa kundi la Islamic State (IS) wamewaua askari polisi wasiopungua 12 wa Iraq katika mashambulizi yalioendeshwa Jumapili hii dhidi ya kambi ya jeshi, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wakijihami kwa bunduki na mabomu, washambuliaji hao wa kundi la IS waliingia usiku wa manane katika kambi ya jeshi ya Speicher, karibu na mji wa Tikrit.
Wapiganaji hao wa kundi la Islamic State "walichukulia ukungu kwa kuingia katika kambi ya Speicher", amesema Mahmoud al-Sorchi, msemaji wa kikosi cha jeshi kiliokua kikipewa mafunzo katika kambi hiyo kwa lengo la kurejesha maeneo waliopoteza katika jimbo la Ninawi (kaskazini ).
Askari polisi "waliweza kuua washambuliaji saba lakini watatu kati yao waaweza kulipua vilipuzi walivyokua wamevalia", ameongeza Mahmoud al-Sorchi, akibaini kwamba maafisa watatu walikuwa miongoni mwa askari polisi waliouawa. Askari polisi ishirini pia walijeruhiwa.
Kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio hilo. Islamic State imesema kuwa washambuliaji saba walifaulu kuingia katika kambi kubwa ya jeshi inayopatikana kwenye umbali wa kilomita 160 kaskazini mwa mji wa Baghdad.
Katika tangazo lake liililorushwa hewani, Islamic State imesema washambuliaji wake waliweza kufika katikati ya kambi ambapo wanajeshi wapya 1,200 waliokua wakipewa mafunzo, na kusababisha mapigano ambayo yalidumu masaa manne.
Kundi la Islamic State liliwahi kudhibiti sehemu moja ya kambi ya Speicher wakati wa mashambulizi yake lililoanzisha mwezi Juni 2014 katikati na kaskazini mwa Iraq. Kundi hilo linatuhumiwa kuwaua vijana zaidi ya 1,700 waliokua walisajiliwa katika jeshi, kulingana na makadirio ya juu. Karibu miili 600 ilizikwa na serikali na vikosi vya washirika baada ya kuuteka mji wa Tikrit mwezi Aprili mwaka 2015.
Kundi la Islamic State hivi karibuni lilikiona cha mtima kuni nchini Iraq na kupoteza udhibiti wa mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la magharibi la Anbar, uliorejeshwa mikoni mwa jeshi la Iraq mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2015.