IRAQ-MASHAMBULIZI-USALAMA

Iraq: mashambulizi dhidi ya Misikiti miwili

Askari polisi wa Iraq afanya uchunguzi katika Msikiti wa Ammar bin Yasser katika mji wa Hilla, kilomita 80 kusini mwa Baghdad, uliolemngwa na shambuli la bomu.
Askari polisi wa Iraq afanya uchunguzi katika Msikiti wa Ammar bin Yasser katika mji wa Hilla, kilomita 80 kusini mwa Baghdad, uliolemngwa na shambuli la bomu. AFP/AFP

Misikiti miwili ya Masuni nchini Iraq imelengwa Jumatatu hii na mashambulizi ya mabomu na shambulio la tatu limemua Muazini, wakati ambapo mauaji ya mhubiri wa Kishia yaliotekelezwa na utawala wa Kisuni wa Saudi Arabia yanatia hofu ya kuzuka vurugu kati ya jamii hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa polisi na madaktari, watu watatu wamejeruhiwa katika mashambulizi dhidi ya Misikiti miwili katika mkoa wa Hilla, katikati mwa Iraq na Muazini ameuawa karibu na nyumbani kwake katika mji wa Iskandariyah, pia katikati mwa nchi hiyo. Hakuna kundi hata moja limedai kuhusika na mashambulizi haya.

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, kutoka jamii ya Mashia kama idadi kubwa ya raia nchini Iraq, ameahidi kwenye Twitter kwamba wahusika wa mashambulizi hayo watakamatwa, akilinyooshea kidole kundi la Islamic State (IS), ambalo linaundwa na watu kutoka jamii wa Masuni.

"Tumeamuru vikosi vya Iraq kuwasaka majambazi wa kundi la IS na washirika wao, ambao wamelenga Misikiti hiyo ili kukuza shuki na kudhoofisha umoja wa kitaifa", amesema Waziri mkuu wa Iraq tweet.

Wizara ya mambo ya ndani imewashutumu "watu walioingia nchini humo" kuendesha mashambulizi hayo " ili kukuza vurugu kati ya jamii za Mashia na Masuni baada ya matukio ya hivi karibuni katika Ukanda huo", akimaanisha dhahiri mauaji ya mhubiri wa Kishia nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa polisi na madaktari, watu waliovalia sare za kijeshi wamelipua mabomu katika misikiti miwili.