YEMENI-HAKI-MAUAJI

Yemen: mwanamke mmoja auawa kwa kupigwa mawe

Wanawake katika mitaa ya mji wa Sanaa, Septemba 1, 2015.
Wanawake katika mitaa ya mji wa Sanaa, Septemba 1, 2015. AFP/AFP/

Wanajihadi wa Al Qaeda nchini Yemen wamempiga mawe hadi kufa mwanamke mmoja baada ya kutuhumiwa "uzinzi" na "ukahaba" katika mji wa Moukalla (kusini) unaodhibitiwa na kundi hilo, mashahidi kadhaa wamesema Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

Kisa hicho kilitokea Jumapili mwishoni mwa juma lililopita, kwa mujibu wa mashahidi hao.

Watu wenye silaha "walimuwekwa mwanamke huyo katikati mwa shimo katikati ya ua la jengo la kijeshi na walipiga mawe hadi kufa mbele ya wakazi kadhaa wa mji" wa Moukalla, mji mkuu wa jimbo la Hadramout, shahidi mmoja ameeleza.

Wanajihadi wa al-Qaeda walichukulia hali ya machafuko nchini Yemen ili kuuteka mji wa Moukalla mwezi Aprili ambako wameweka sheria zao.

Jumapili, wanajihadi hao walimpiga mawe mwanamke huyo wakitaja uamuzi uliochukuliwa Desemba 8 na "Mahakama ya Kiislamu" ya al-Qaeda katika jimbo la Hadramout, Mahakama ambayo waliunda wenyewe. Mahakama hiyo imesema kuwa mwanamke huyo, ambaye alikuwa aliolewa, "alikiri mwenyewe mbele ya majaji kuwa alikua akijihusisha na uzinzi."

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamke huyo alikuwa pia alihukumiwa na wanajihadi kujihusisha na "ukahaba" pamoja na "uzinzi", vile vile alikua "akitumia hashish", aina ya kilevi.

Mwandishi wa habari wa Yemen, ambaye alikuepo wakati mwanamke huyo alipigwa mawe hadi kufa, amesema kuwa watu wenye silaha walikataza kupiga picha.