IRAQ-IS-SHAMBULIO

Iraq: wapiganaji 25 wanaounga mkono serikali wauawa

Vikosi vinavyoiunga mkono serikali na Idara zinazopambana dhidi ya ugaidi nchini Iraq wakati wa mapigano dhidi ya kundi la IS katika harakati za kukuchukua udhibiti wa maeneo yote ya mji wa Ramadi, Januari 4, 2016.
Vikosi vinavyoiunga mkono serikali na Idara zinazopambana dhidi ya ugaidi nchini Iraq wakati wa mapigano dhidi ya kundi la IS katika harakati za kukuchukua udhibiti wa maeneo yote ya mji wa Ramadi, Januari 4, 2016. AFP/AFP/

Wapiganaji wasiopungua 25 wa vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Iraq wameuawa wakati walipokua wakizima shambulizi kubwa lililokua likiendeshwa na kundi la Islamic State (IS) katika mji wa Haditha, katika jimbo la magharibi la Al-Anbar, vyanzo vya usalama vimearifu Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili lilianzishwa Jumapili wakati ambapo mwezi Desemba kundi la IS lilipoteza udhibiti wa mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la Al-Anbar, kilomita 80 kusini mwa mji wa Haditha baada ya mashambulizi ya vikosi vinavyoiunga mkono serikali.

"Tumepoteza mashujaa 25 ndani ya masaa 72", mkuu wa vikosi vya kikabila, Sheikh Abdalla Atallah, amesema alipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP kutoka Haditha, eneo ambapo kunapatikana bwawa la pili kwa ukubwa nchini Iraq na ambalo linakabiliana na mashambulizi ya kundi la IS tangu mwaka 2014.

"Ni moja ya mashambulizi makubwa dhidi yetu", ameeleza Sheikh Abdalla Atallah, akibaini kwamba watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Meya wa mji wa Haditha, mji unaopatikana kwenye kilomita 200 kaskazini magharibi mwa mji wa Baghdad, amethibitisha idadi hiyo ya wapiganaji waliouawa. "Tuna zaidi ya mashujaa 20 na zaidi ya wengine 50 wamejeruhiwa", Mabrouk Hamid amesema, akibaini kwamba waliouawa ni kutoka jeshi, Idara zinazopambana dhidi ya ugaidi, polisi pamoja na wapiganaji wa kikabila.

Hamid amesema kwamba shambulio hilo "limeyashirikisha magari 40 ya kivita, huku baadhi ya magari hayo yakijazwa vilipuzi."