SYRIA-MISAADA

Syria: misaada ya kibinadamu yaingia Madaya

Msafara wa magari yanayobeba misaada ya Shirika la Msalaba Mwekundu yakiingia katika mji wa Madaya nchini Syria, Januari 11, 2015.
Msafara wa magari yanayobeba misaada ya Shirika la Msalaba Mwekundu yakiingia katika mji wa Madaya nchini Syria, Januari 11, 2015. AFP/AFP

Msafara wa magari yanayobeba misaada ya kibinadamu umewasili Jumatatu hii mchana katika mji wa waasi wa Madaya karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus.

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Madaya umezingirwa kwa miezi sita sasa na jeshi la Syria na raia iwameendelea kukabiliwa na njaa kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu.

"Malori mawili yaliobeba chakula na chanjo na mengine yaliojaa vifaa vingine vya kujikinga na baridi yameingia saa 11:00 jioni (sawa na 9:00 alaasiri sa za kimataifa) katika mji wa Madaya", afisa wa shirika la Msalaba mwekundu nchini Syria (SARC) ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wakati huo huo, malori matatu yameingia katika mji wa Foua na mengine matatu katika mji wa Kafraya, maeneo mawili yanayokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia yanayozingirwa na waasi, kilomita 300 kutoka mji wa Damascus, katika jimbo la Idleb (kaskazini magharibi mwa Syria), kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi kilio eneo hilo.

Awali msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu (ICRC) alisema, malori 44 yamekua njiani yakielekea katika mji wa Madaya, karibu na mji wa Damascus, na malori 21 yamekua njiani yakielekea katika maeneo ya Foua na Kafraya, kaskazini mwa Syria, maeneo mabayo yanadhibitiwa na waasi.

Magari hayo yanabeba chakula, dawa, blanketi lakini pia kwa sababu vifaa mbalimbali vyakujikinga na baridi, kwani wakazi wa maeneo hayo, yanayozingirwa kwa miezi, wamenyimwa hai ya kila kitu na hali kwa sasa ni mbaya zaidi.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasio na mipaka (MSF), watu wasiopungua 23 wamefariki kutokana na njaa katika mji wa MAdaya.