SYRIA-UN_MISAADA

Syria: raia wanaokabiliwa na njaa mbioni kuondolewa kutoka Madaya

Wanawake na watoto waliokusanyika katika kitongoji cha Madaya Januari 11, 2016, Syria.
Wanawake na watoto waliokusanyika katika kitongoji cha Madaya Januari 11, 2016, Syria. AFP/AFP

Mamia ya raia ambao wako "katika hatari ya kupoteza maisha" wnaweza kuondolewa Jumanne hii kutoka Madaya, mji wa Syria unaozingirwa kwa miezi sita na jeshi ambapo baadhi ya wakazi wa mji huo wanakabiliwa na njaa, mkuu wa operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa alitangaza Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Mslaba Mwekundi nchini Syria limesema msafara wa malori 44 ya yaliokua yakisafirisha chakula, dawa na blanketi yaliiingia Jumatatu katika mji wa Madaya. Katika mji huu wa Madaya, watu 28 walifariki kutokana na njaa tangu Desemba 1, kwa mujibu wa shirika sisilo la kiserikali Madaktari wasio na mipaka (MSF).

Jumla ya raia 400,000 wako katika miji ya Syria inyozingirwa na jeshi la serikali la serikali ya Bashar al-Assad au waasi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

"Watu 400 wataondolewa mara moja katika mji wa Madaya" kwa sababu "wako katika hatari ya kupoteza maisha," kutokana na maradhi mbalimbali yanayowakabili, hususan utapiamlo au "matatizo mengine ya kiafya" na Umoja wa Mataifa unatarajia zoezi hilo kuanza labda mapema Jumanne, alisema Stephen O'Brien, mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na operesheni za kibinadamu.

Bw O'Brien aliwasilisha ripoti ya hali inayojiri katika mji wa Madaya na miji mingine nchini Syria inayozingirwa kwa mabalozi wa nchi 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,waliokutana kwa faragha.Balozi Uhispania Roman Ozargun Marchesi kisha alikumbusha kwamba "kuzingira (raia) kwa lengo la kuwaweka katika hali ya njaa ni uhalifu wa kivita."