SYRIA-UN-MISAADA

Syria: Ban Ki-moon alaani kuzingirwa kwa miji kama "uhalifu wa kivita"

Mji waasi wa Madaya, kusini magharibi mwa Syria, umezingirwa kwa miezi sita na jeshi la Bashar Al Assad.
Mji waasi wa Madaya, kusini magharibi mwa Syria, umezingirwa kwa miezi sita na jeshi la Bashar Al Assad. REUTERS/Omar Sanadiki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza Alhamisi kwa kukemea uhalifu wa kivita unaoendelea kushuhudiwa kwa kuzingirwa miji mbalimbali ya Syria, hususan mji wa Madaya, ambapo raia wanakabiliwa na njaa.

Matangazo ya kibiashara

Ban Ki-moon ameinyooshea kidole serikali ya Syria kuhusu uhalifu huo. Pia ameulenga upinzani dhidi ya Bashar Al-Assad. Lugha isiyo ya kawaida ya Ban Ki-moon kwa kutaka kuongeza shinikizo kwa pande mbili kujadili mpango wa amani kuanzia Januari 25 katika Geneva.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu mjini New York, Marie Bourreaum, hii ni mara ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kupitia sauti ya Katibu Mkuu wake kuonyesha pia msimamo ulio wazi kuhusu hatima ya miji inayozingirwa nchini Syria. "Hebu tuwe wa kweli: matumizi ya njaa kama silaha ya vita ni kosa la jinai", Ban Ki-moon amesema Alhamisi hii. Pande zote, ikiwa ni pamoja na serikali ya Syria ambayo ina majukumu ya kulinda raia wa Syria, inahusika kwa mauaji haya na makosa mengine yanayopigwa marufuku na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Mataifa ya Ukanda na kwingineko, ambayo yanaweza kuwa na ushawishi, yanapaswa kuzishishinikizo pande zote ili kupata haki ya kuwafikilia raia ili kuweza kuwahuduma. "

Umoja wa Mataifa waongeza shinikizo

Shinikizo hili la Umoja wa Mataifa litaongezeka zaidi kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa hii. Baraza hili lina matumaini ya kupata kile linachoita "hatua za matumaini" kwa kufuta hatua ya kuzingira maeneo mbalimbali na kuboresha hatma ya raia, na hayo yote, katika siku kumi na moja ya mwanzo wa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Syria na upinzani.

Umoja wa Mataifa haujachukua hatua ya kuiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kuanzisha utaratibu wa kuwashughulikia wanaohusika na uhalifu wa kivita nchini Syria.

Msafara wa magari yanayobeba msaada wa kibinadamu

Baada ya msafara wa kwanza wa magari yanayobeba msaada wa kibinadamu kuwasili Jumatatumwanzoni mwa wiki hii katika miji mbalimbali inayozingirwa , Alhamisi hii msafara wa pili wa magari 44 yanayobeba chakula na dawa yaliingia katika mji wa Madaya, kilomita arobaini kutoka mji wa Damascus kwa kuwaokoa wakazi wanaokabiliwa na na njaa.