AFGHANISTAN-SHAMBULIO

Shambulio karibu na ubalozi wa Urusi Kabul

Askari polisi wa Afghanistan wakiwasili kwenye eneo la shambulio lililotokea, Kabul Desemba 11, 2015.
Askari polisi wa Afghanistan wakiwasili kwenye eneo la shambulio lililotokea, Kabul Desemba 11, 2015. REUTERS/Omar Sobhani

Wafanyakazi angalau saba wa runinga ya moja ya Afghanistan Tolo wameuawa Jumatano hii katikati mwa mji wa Kabul katika shambulio kubwa la kwanza la kigaidi dhidi ya moja ya vyombo vya habari nchini Afghanistan na kuwajeruhi pia watu 25.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna kundi hata moja ambalo limeshadai kuhusika na shambulio hilo la bomu lililotegwa katika gari lakini, kundi la Taliban lilitangaza mwezi Oktoba kwamba vituo vikuu viwili vya televisheni nchini Afghanistan Tolo na 1TV, vinapaswa "kulengwa kwa mashambulizi ya kijeshi". Kundi hili limekua likivishutumu vituo hivi kupeperusha hewani "propaganda" za serikali na kuthibitisha kwamba waasi wa Kiislam walifanya ubakaji wakati wa mapigano katika mji wa Kunduz (kaskazini) uliovamiwa na wapiganaji mwezi Septemba mwaka jana.

Jumatano hii basi la lililokiwasafirisha wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji Kaboora, kampuni tanzu ya shirika la Tolo linalomiliki rmoja ya runinga kuu nchini Afghanistan Tolo. Tolo ni sehemu ya Moby Group, ambayo ni mali ya Saad Mohseni, tajiri maarufu anayemiliki vyombo kadhaa vya habari.

Tangu mwanzoni mwa mwaka, mji wa Kabul umelengwa mpaka sasa na mashambulizi anagalau sita. Roketi moja ilianguka karibu na ubalozi wa Italia mjini Kabul siku ya Jumapili, na kuwajeruhi walinzi wawili.

Mashambulizi yanatokea sanjari na jitihada mpya za kuendelea na mchakato wa amani pamoja na kundi laTaliban, mchakato ambao ulikatishwa mwezi Julai mwaka jana. Wajumbe wa Afghanistan, Pakistan, China na Marekani, ambao walikutana mapema wiki hii katika mji mkuu wa Afghanistan ili kutazama kwa pamoja jinsi ya kuanzisha upya mazungumzo hayo, wamelitolea wito kundi la Taliban kujiunga kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya amani.