SYRIA-IS-MAUAJI

Syria: watu zaidi ya 30, wauawa katika mashambulizi mashariki

mji wa Deir Ezzor en Syrie, Januari 4, 2016.
mji wa Deir Ezzor en Syrie, Januari 4, 2016. AFP/AHMAD ABOUD/AFP

Watu wasiopungua 30, wakiwemo watoto 13, wameuawa Ijumaa hii katika jimbo la Syria la Deir Ezzor (Mashariki mwa Syria) katika mashambulizi ya anga yalioendeshwa na serikali ya Syria au na ndege za Urusi, shirika la Haki za binadamu nchini Syria ( OSDH) limebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Watu thelathini, ikiwa ni pamoja na wanawake 8 na watoto 13, waliuawa katika eneo la Tabiya Jazeera (kilomita 20 mashariki mwa mji wa Deir Ezzor) na ndege za jeshi la serikali au za jeshi la Urusi", OSDH imesema.

Deir Ezzor ni jimbo lenye utajiri wa mafuta ambalo liko mikononi mwa kundi la Islamic State (IS), ispokua nusu ya mji mkuu wa mkoa na uwanja wa ndege, ambavyo viko mikononi mwa serikali.

Katika siku za hivi karibuni, kundi la Islamic State liliimarisha ulinzi katika mji wa Deir Ezzor baada mashambulizi lililoendesha Jumamosi juma lililopita. Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu kadhaa kwa pande zote mbili na miongoni mwa raia. Wakati huo wapiganaji wa kundi la IS waliwateka nyara raia 130.

Kwa mujibu wa shirika la Haki za binadamu la Syria (OSDH), watu wasiopungua 439 wamepoteza maisha katika jimbo la Deir Ezzor tangu Jumamosi juma lililopita, katika mapigano, mashambulizi ya anga na mauaji ya raia pamoja na wapiganaji wa naounga mkono serikali. Kundi la IS linanyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo.