ISRAEL-PALESTINA-MASHAMBULIZI

Ukingo wa Magharibi: Wapalestina 2 wauawa

Askari wa Israel wakipiga doria karibu na kijiji cha Palestina kusini mwa Ukingo wa Magharibi, Januari 18, 2016.
Askari wa Israel wakipiga doria karibu na kijiji cha Palestina kusini mwa Ukingo wa Magharibi, Januari 18, 2016. AFP/AFP

Wapalestina wawili wamewajeruhi Jumatatu hii kwa kisu wanawake wawili wa Isarel, ambapo mmoja amejeruhiwa vikali, katika makazi ya Waisrael katika Ukingo wa Magharibi, kabla ya kuuawa kwa risasi, polisi ya Israel na Idara ya huduma za dharura wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Watu wawili waliwadunga kisu wanawake wawili, wenye umri wa mika 40 na 58, katika mj9 wa Beit-Horon, kaskazini magharibi mwa Jerusalem, polisi imesema.

Mmoja wa wanawake hao yuko katika hali mbaya, mwengine amepata majeraha madogo, Idara ya huduma za dharua imebaini. Washambuliaji wawili wameuawa kwa risasi na walinzi wa mji huo, polisi imeongeza.

Mabomu mawili yaliteguliwa katika eneo la tukio, jeshi na polisi wamesema.

Hili ni shambulio la tatu katika mji wa Beit-Horon kwa muda wa siku nane wakati ambapo maeneo ya Ukingo wa Magharibi, Jerusalem na Israeli vinaendelea kukumbwa na vurugu ambazo zimesababisha vifo vya Wapalestina 159 na Waisrael 24 tangu Oktoba 1, kulingana na takwimu za shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wengi wa Wapalestina waliouawa ni wahalifu au washukiwa wa mashambulizi.

Raia mmoja wa Marekani na mwengine mmoja kutoka Eritrea pia waliuawa katika ghasia hizo.