SYRIA-UN-MAZUNGUMZO

Serikali ya Syria yaidhibiti upya ngome ya waasi

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura. Reuters/路透社

Jeshi la Syria limeidhibiti upya ngome ya waasi siku chache kabla ya mazungumzo pamoja na upinzani. Jumanne hii serikali ya Bashar Al Assad inatazamiwa kuamua iwapo itashiriki au la katika mazungumzo hayo, yenye lengo la kupata ufumbuzi wa mgogoro unaoendelea kushuhudiwa nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura ametangaza kwamba ametuma mialiko kwa "wajumbe mbalimbali kutoka Syria" watakaoshiriki mazungumzo hayo Ijumaa wiki hii, bila hata hivyo kubainisha watu watakao shiriki mazungumzo hayo. Hata hivyo bado hawajaafikiana kufusu muundo wa ujumbe wa upinzani.

Vikisaidiwa na ndege za Urusi, wapiganaji wa Hezbollah kutoka Lebanon na maafisa wa Iran, vikosi vya serikali vimeudhibiti Jumatatu hii jioni mji wa Sheikh Miskine katika mkoa wa kusini wa Deraa, karibu na mpaka wa Jordan.

Huu ni ushindi muhimu, mji huo ulikua eneo muhimu linaloelekeza kaskazini mwa Damascus na mashariki ya mji wa Suweida, maeneo ambayo bado ipo mikononi mwa serikali, ingawa sehemu kubwa ya jimbo la Deraa bado inashikiliwa na waasi, ikiwa ni pamoja na waasi wa kundi la Al-Nosra Front, tawi la Al Qaeda nchini Syria.

Urusi, ambaye ni mshirika wa serikali iliyoingilia kati kijeshi Septemba 30 katika vita nchini Syria, imekaribisha hatua kutokana na msaada wake ambao umepelekea vikosi vya usalamnakuyadhibiti maeneo kadhaa yaliyokuwa mikononi mwa waasi.

Lakini majeshi ya serikali ya Bashar Al Assad yanaendelea kupata pigo kubwa kutoka kwa wapiganaji wa makundi ya Kiislamu, baada ya shambulio jipya la kujitoa mhanga lilodaiwa kutekelezwa na kundi la IS kugharimu maisha ya watu wasiopungua 22, wengi wakiwa ni askari, katika mji wa kati wa Homs.

Kwa upande wake Uturuki imesema hatoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Syria yatakayoanza mjini Geneva siku ya Ijumaa kama chama cha PYD cha Wakurdi kutoka Syria hakitoshiriki, ameonya Jumanne hii Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.