SYRIA-MAREKANI-URUSI

Syria: mashaka na tofauti kwa mkataba wa usitishwaji mapigano

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri wake wa Mambo ya Nje John Kerry, wakati wa hotuba, Alhamisi, Februari 25, baada ya kukutana na Baraza la Usalama la UN.
Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri wake wa Mambo ya Nje John Kerry, wakati wa hotuba, Alhamisi, Februari 25, baada ya kukutana na Baraza la Usalama la UN. REUTERS/Carlos Barria

Urusi na Marekani zimeongeza shinikizo kwa washirika wao katika vita vinavyoendelea nchini Syria ili kuheshimisha mkataba wa usitishwaji wa mapigano ambao unatazamiwa kuanza kutekelezwa Jumamosi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Umoja wa Mataifa unatazamiwa kujadili Ijumaa hii rasimu ya azimio ambalo litaidhinisha makubaliano juu ya usitishwaji wa mapigano. Lakini wahusika wakuu kuu katika mgogoro wa Syria wameendelea kugawanyika. Baadhi wanaikubali, na baadhi wanaikataa na karibu wote wamejizuia kuonyesha msimamo wao. Ispokua Urusi, ambayo ina matumaini na mara kwa mara inasema hakuna njia nyingine mbadala.

Wakubali au la mkataba huo wa usitishwaji wa mapigano, wahusika wakuu katika mgogoro wa Syria wanakubaliana jambo moja: kama kweli mkataba wa usitishwaji wa mapigano utatekelezwa, hauhusu kamwe makundi ya kijihadi.

Nchi zote zinazohusika nchini Syria zimekua zikiendesha mashambulizi ya mabomu dhidi ya ngome za makundi ya Islamic State na Al-Nusra Front. Lakini uwezekano wa utekelezaji wa mkataba huu ni kama ndoto, wakati ambapo pande zote zimegawanyika.

Upinzani nchini Syria, umetoa masharti yake kwa mkataba huo wa usitishwaji wa mapigano, ukisema kuwa masharti ya kuuheshimu hayajawekwa sawa. Hatimaye upinzani huu ulikubali kwa shinikizo la Marekani. Umekubali lakini kwa muda mdogo: siku 15.

Serikali ya Syria pia imekubali pendekezo la Moscow. Assad ameahidi kuheshimu mkataba wa usitishwaji wa mapigano lakini ataendelea kulenga "magaidi." Kwa upande wa serikali ya Damascus, neno hili linahusu wanajihadi pamoja na waasi wanaojiita wa wastani.