SYRIA-MAPIGANO-MKATABA

Syria: pande mbili zatuhumiana kukiuka mkataba

Magari yakionekana katika mitaa ya mji Damascus baa ya mkataba wa usitishwaji wa mapigano kuanza kutekelezwa Februari 27, 2016.
Magari yakionekana katika mitaa ya mji Damascus baa ya mkataba wa usitishwaji wa mapigano kuanza kutekelezwa Februari 27, 2016. Sameer Al-Doumy/AFP

Wahusika wakuu kuu katika mgogoro wa Syria wameshutumiana Jumapili hii kila mmoja kukiuka mkataba wa usitishwaji wa mapigano ulioanza kutekelezwa Jumamosi hii, huku wakibaini kwamba mkataba huo umeheshimishwa kwa siku ya pili.

Matangazo ya kibiashara

Katika miji mikubwa, watu wameendesha shughuli mbalimbali Jumapili hii asubuhi baada ya kulala usiku kucha katika milio ya risasi na milipuko. Kwa sasa hali ya utulivu imereje, na katika eneo la waasi la Aleppo, wanafunzi ambao wamekua wamezoea kutembea karibu na kuta ili kuepuka mabomu wameonekana Jumapili hii katikati ya barabara, kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Jeneral Sergei Kouralenko, mkuu wa Kituo cha Maridhiano ya pande zinazopigana nchini Syria kinachosimamiwa na Urusi, ameshutumu wapiganaji kukiuka mara tisa makubaliano ya usitishwaji wa mapigano ulioanzishwa na Washington pamoja na Moscow, na kuongeza kwamba "kwa ujumla, mkataba wa usitishwaji mapigano umekua umeshaanza kutekelezwa nchini Syia. "

Wakati huo huo, msemaji wa Kamati Kuu ya mazungumzo (HCN) amebaini kwamba "Jumamosi kulikuwa na visa kumi na tano vya ukiukwaji (wa mkataba wa usitishwaji mapigano) viliotekelezwa na vikosi vya serikali, ikiwa ni pamoja na visa 2 viliotekelezwa na Hezbollah (kundi la wasi wa Kishia kutoka Lebanon) katika mji wa Zabadani" .

Lakini "kwa ujumla ni bora zaidi kuliko kabla na watu wanajisikia vizuri," amesema Salem al-Meslet kutoka mjini Riyadh, ambapo HCN inaendeshea harakati zake.

Saudi Arabia, ambayo inaunga mkono upinzani wa Syria, kwa upande wake, imeishtumu "ndege za kivita za Urusi na zile za utawala wa Syria" kwa kukiuka mkataba wa usitishwaji wa mapigano.

Ndege za kijeshi ziliendesha mashambulizi Jumapili hii alfajiri katika maeneo sita ya jimbo la Aleppo (kaskazini mwa Syria) na lile la Hama (katikati mwa Syria), kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Rami Abdel Rahman, amesema mashambulizi hayo ya anga yameua mtu mmoja. Amebaini kwamba, moja ya vijiji viliolengwa, Kafar Hamra, kinadhibitiwa na wanajihadi wa Al-Nusra Front, tawi la kundi la Al Qaeda nchini Syria. Vijiji vingine viko mikono ya waasi lakini wapiganaji wa kjihadi wako katika maeneo jirani.

Mkataba wa usitishwaji wa mapigano unahusu tu maeneo kunakoripotiwa mapigano kati ya vikosi vya utawala wa Syria, vinavyosaidiwa na mshirika wake Urusi, na waasi wa Syria na hauwahusu makundi ya wanajihadi Islamic State (IS) na Al-Nosra Front, ambayo yanadhibiti zaidi ya 50% yaardhi ya Syria.