SYRIA-UN-MAZUNGUMZO

Syria: mazungumzo kuanza Machi 10

Mashambulizi mawaili ya anga yameendeshwa Machi 4, 2016 karibu namji wa Douma, eneo la waasi mashariki mwa Damscus, mji mkuu wa Syria.
Mashambulizi mawaili ya anga yameendeshwa Machi 4, 2016 karibu namji wa Douma, eneo la waasi mashariki mwa Damscus, mji mkuu wa Syria. AFP

Duru mpya ya mazungumzo ya amani baina ya wadau wote nchini Syria yanatazamiwa kuanza tarehe 10 Machi mjini Geneva, wahusika katika mazungumzo hayo wameanza kuwasili, amesema mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura katika mahojiano yaliyochapishwa Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Amekumbusha kwamba mchakato wa ufunbuzi wa mvutano wa kisiasa nchini Syria, ambapo zaidi ya watu 270,000 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vita hivyo mwezi Machi 2011, utapelekea kuundwa kwa serikali mpya, kuandaa katiba mpya na kufanyika kwa uchaguzi.

tarehe ya mazungumzo hayo, ambayo ni ya pili ya aina hiyo mwaka huu, iliahirishwa kutoka 07 hadi 09 Machi kwa ajili ya maswali ya vifaa.

"Nia yetu ni kuanzisha mchakato tangu Machi 9 mchana," Bw de Mistura amesema katika gazeti la kiarabu la kila la Al-Hayat.

Lakini, amesema, "Nadhani tutaanza tarehe 10. Ni katika hatua hii ambapo mchakato utaanza," kulingana na tafsiri ya Kiarabu ya gazeti hilo.

Mjumbe maalum amesema kuwa "baadhi ya washiriki watakua wamewasili tarehe 9. Wengine, kutokana na matatizo ya kupata vyumba hotelini watafika tarehe 11 na wengine tarehe 14."

De Mistura amesema mazungumzo yatafanyika kama yale yaliotangulia, hapana moja kwa moja.

"Mikutano ya matayarisho itafanyika, kisha tutafanya majadiliano ya kina na kila upande tofautijuu ya masuala muhimu," amesema de Mistura.

Alisisitiza zaidi kuwa "agenda ya mchakato (udhibiti) iko wazi: Kwanza mazungumzo kwa ajili ya kuundwa serikali mpya, jambo la pili katiba mpya na jambo la tatu uchaguzi wa wabunge na urais ndani ya miezi 18" .

Duru ya kwanza ya mazungumzo ilikuwa ilisitishwa mapema mwezi Februari kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi nchini Syria. Moscow inaongoza kampeni ya mashambulizi ya anga tangu mwezi Septemba kwa kuusaidia utawala wa Bashar al-Assad.

Tangu wakati huo makubaliano juu ya usitishwaji wa uhasama ulijadiliwa na na kuhitimishwa na Marekani pamoja na Urusi, kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.

Lakini upinzani nchini Syria bado unasita kushiriki katika mazungumzo ya mjini Geneva, ukisema kuwa hali bado ni tete.