UAE-MAFURIKO

UAE yakumbwa na mafuriko

Vifaa vingi vikiharibika baada ya mvua kubwa zenye upepo kunyesha Abu Dhabi, Machi 9, 2016.
Vifaa vingi vikiharibika baada ya mvua kubwa zenye upepo kunyesha Abu Dhabi, Machi 9, 2016. AFP

Mvua kubwa zisio za kawaida zimenyesha Jumatano hii katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchi ya jangawani katika Ghuba, na kusababisha mafuriko. Hali hii imesababisha shule zote nchini humo kufungwa na safari za ndege kuzorota.

Matangazo ya kibiashara

Shule zitaendele kufungwa Alhamisi hii, mamlaka ya Hali ya Hewa imebaini kwamba kuna hatari mvua hizi zenye upepo mkubwa ziendelea kunyesha kwa siku kadhaa nchini humo, Wizara ya Elimu imesema katika taarifa yake..

Mafuriko haya ni nadra sana katika Umoja wa Falme za Kiarabu, moja ya nchi kumi zenye ukami duniani. Milimita 240 ya maji ya mvua yameshuhudiwa karibu na mji wa Al-Ain, wakati ambapo kiwango cha wastani kwa mwaka ni mililita 78 nchini humo, sawa na zaidi ya mara 15 chini ya Uingereza, kwa mujibu wa mamlaka ya Hali ya Hewa.

Picha ziliorushwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha miti iking'olewa, maeneo ya kuegesha magari yakiharibiwa na magari mengi nusu yakizama ndani ya maji yaliofurika za mji wa Abu Dhabi.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi ilisitisha safari zote za ndege kabla ya kutangaza safari hizo kuanza tena mapema mchana, wakati ambapo safari nyingi zimecheleweshwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, kwa mujibu wa mamlaka ya usafiri wa anga.

Shuguli nyingi zimezorota katika maeneo mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, huku polisi ikibaini kwamba imeorodhesha ajali zaidi ya 250 za barabarani ziliosababishwa na mvua hizo, kwa siku tuu ya Ijumatano hii.