SYRIA-UPINZANI-MAZUNGUMZO

Syria: mazungumzo kati ya serikali na upinzani kuanza leo

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura mbele ya hoteli ya Rais Wilson mjini Geneva, Februari 3, 2016.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura mbele ya hoteli ya Rais Wilson mjini Geneva, Februari 3, 2016. REUTERS/Denis Balibouse

Mazungumzo kati ya serikali ya Syria na upinzani unaojumuika katika Kamati Kuu ya Mazungumzo (HCN) yanaanza Jumatatu hii Machi 14 mjini Geneva. Pande zote husika katika mazungumzo hayo zimewasili mjini Geneva kushiriki mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Kamati Kuu ya Mazungumzo (HCN), ambayo inaleta pamoja makundi muhimu ya upinzani nchini Syria, imesema Jumapili hii kwamba upinzani umewasili mjini Geneva kushiriki mazungumzo.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Ijumaa wiki iliyopita, HCN ilisema kwamba watashiriki katika mazungumzo chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, kwa kuzingatia "dhamira yake ya kushirikiana na juhudi za kimataifa za kukomesha umwagaji damu na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa" kwa mgogoro wa Syria.

Hivi karibuni Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura alitangaza kuwa "majadiliano makubwa yataanza Machi 14 hadi Machi 24 au kabla ya terehe hiyo."

Ujumbe wa serikali ya Syria, ukiongozwa na balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar al-Jaafari, uliwasili Jumapili hii asubuhi mjini Geneva.

Katika taarifa yake, HCN ilisema kwamba ingeliweza kuzungumzia "kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito yenye mamlaka zote za utawala" ambapo Rais Bashar al-Assad "hatopewa nafasi hata moja."

HCN inasema kwamba "haitoi masharti yoyote kwa kushiriki katika mazungumzo," lakini inasisitiza kuwa pande husika zinatakiwa kujiunga kwenye mikataba ya kimataifa juu ya masuala ya kibinadamu.

Mratibu Mkuu wa HCN Riad Hijab amesema kuwa ujumbe wake uko tayari "kutumia fursa zote ili kupunguza mateso yanayowakabili raia wa Syria."

Hatahivyo serikali ya Damascus imesema hatima ya Rais Bashar Al Assad haipaswi kuwekwa katika ajenda ya mazungumzo ya mjini Geneva, ikitaja kuwa ni "mstari mwekundu".

Washington na Paris wametoa wito Jumapili hii wa kufanyaika kwa mazungumzo ya "kweli" juu ya mabadiliko ya kisiasa nchini Syria, na kufutilia mbali kile serikali ya Syria inasema hatima ya Bashar Al Assad ni "msatri mwekundu" ambao hautakiwi kuwa katika ajenda ya mazungumzo.

Umoja wa Ulaya na Marekani, ambao wamekutana Jumapili hii mjini Paris, pia wamesisitiza juu ya mapigano na utoaji wa misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha mazungumzo yenye "kuaminika", wakati ambapo vita, ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 270,000 na mamilioni ya wakimbizi vikiingia mwaka wake wa sita.

"Pande zote zinapaswa kuheshimu mkataba wa usitishwaji wa mapigano, kushirikiana katika utoaji wa misaada ya kibinadamu, na kuheshimu mchakato wa mazungumzo ili kufikia mabadiliko ya kisiasa. Kama serikali na washirika wake wanafikiri kwamba wanaweza kujaribu kuvunja mipaka (. ..) wanajidanganya," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, baada ya kukutana na wenzake wa Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Italia na Umoja wa Ulaya.

John Kerry pia amekosoa hotuba aliotoa siku moja kabla mwenzake wa Syria Walid Muallem, ambaye alifutilia mbali katika mazungumzo ya Geneva kuzungumzia hatima ya Rais Bashar Al Assad, suala alilolitaja kuwa ni "mstari mwekundu."

Muallem "anajaribu waziwazi kukwepesha mchakato," amelaani Bw Kerry, akiungwa mkono na mwenzake wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault, ambaye amebaini kwamba ni "uchokozi".

"Kuna umuhimu wa kutekeleza mabadiliko ya kisisasa ya kweli. Hili ndilo litakua katika ajenda ya mazungumzo mjini Geneva," amesema Bw Ayrault, akirejelea "kurudi kwa hali kama ilivyo" inapaswa kufutiliwa mbali. "Tunahitaji mambo yabadilike," Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa amesema.

Mkataba wa usitishwaji mapigano na misaada ya kibinadamu

Mazungumzo ya Geneva yanapaswa kushughulikia kwa mara ya kwanza katika njia thabiti mustakabali wa nchi, baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo iliofeli mwezi Januari mjini Geneva, kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi na hali mbaya ya kibinadamu.

Mazungumzo haya mpya, hata yanaonekana kuwa "magumu", yanaanza katika hali ya misimamo tofauti.

Zaidi ya watu 270,000 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vita nchini Syria, Machi 15, 2011,