SYRA-MAZUNGUMZO-USALAMA

Syria: Washington na Paris waomba kufanyika kwa mazungumzo ya “kweli”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault (kushoto) na mwenzake wa Marekani John Kerry katika mkutano Quai d'Orsay (wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa) Machi 13, 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault (kushoto) na mwenzake wa Marekani John Kerry katika mkutano Quai d'Orsay (wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa) Machi 13, 2016. GONZALO FUENTES/POOL/AFP

Washington na Paris wametoa wito Jumapili hii wa kufanyaika kwa mazungumzo ya "kweli" juu ya mabadiliko ya kisiasa nchini Syria, na kufutilia mbali kile serikali ya Syria inasema hatima ya Bashar Al Assad ni "msatri mwekundu" ambao hautakiwi kuwa katika ajenda ya mazungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo zimesalia tu saa chache ili mazungumzo mapya kati ya serikali ya Damascus na upinzani yaanze mjini Geneva Jumatatu hii Machi 14.

Umoja wa Ulaya na Marekani, ambao wamekutana Jumapili hii mjini Paris, pia wamesisitiza juu ya mapigano na utoaji wa misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha mazungumzo yenye "kuaminika", wakati ambapo vita, ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 270,000 na mamilioni ya wakimbizi vikiingia mwaka wake wa sita.

"Pande zote zinapaswa kuheshimu mkataba wa usitishwaji wa mapigano, kushirikiana katika utoaji wa misaada ya kibinadamu, na kuheshimu mchakato wa mazungumzo ili kufikia mabadiliko ya kisiasa. Kama serikali na washirika wake wanafikiri kwamba wanaweza kujaribu kuvunja mipaka (. ..) wanajidanganya," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, baada ya kukutana na wenzake wa Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Italia na Umoja wa Ulaya.

John Kerry pia amekosoa hotuba aliotoa siku moja kabla mwenzake wa Syria Walid Muallem, ambaye alifutilia mbali katika mazungumzo ya Geneva kuzungumzia hatima ya Rais Bashar Al Assad, suala alilolitaja kuwa ni "mstari mwekundu."

Muallem "anajaribu waziwazi kukwepesha mchakato," amelaani Bw Kerry, akiungwa mkono na mwenzake wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault, ambaye amebaini kwamba ni "uchokozi".

"Kuna umuhimu wa kutekeleza mabadiliko ya kisisasa ya kweli. Hili ndilo litakua katika ajenda ya mazungumzo mjini Geneva," amesema Bw Ayrault, akirejelea "kurudi kwa hali kama ilivyo" inapaswa kufutiliwa mbali. "Tunahitaji mambo yabadilike," Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa amesema.

Mkataba wa usitishwaji mapigano na misaada ya kibinadamu

Mazungumzo ya Geneva yanapaswa kushughulikia kwa mara ya kwanza katika njia thabiti mustakabali wa nchi, baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo iliofeli mwezi Januari mjini Geneva, kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi na hali mbaya ya kibinadamu.

Mazungumzo haya mpya, hata yanaonekana kuwa "magumu", yanaanza katika hali ya misimamo tofauti.