URUSI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA
Ndege ya kwanza ya Urusi yaondoka Syria
Imechapishwa:
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza leo Jumanne kuwa, ndege yake ya kwanza ya kivita imeondoka nchini Syria baada ya agizo la rais Vladimir Putin.
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii inakuja siku moja baada ya rais Putin kutangaza mpango wa kuanza kurudisha nyumbani ndege za kivita wakati huu mazungumzo ya amani yakiingia siku ya pili jijini Geneva nchini Uswizi.
Hata hivyo, rais Putin amesema ndege kadhaa za kivita na wanajeshi watasalia nchini Syria kuendelea kuimarisha usalama.
Imekuwa ikikadiriwa kuwa, Urusi imekuwa kati ya wanajeshi wa ardhini elfu tatu na elfu sita kupambana na wapinzani wa rais Bashar Al Assad.