UTURUKI-SOKA

Uturuki: mchuano kati ya Galatasaray-Fenerbahçe waahirishwa

Polisi ya Uturuki ikipiga doria Machi 20 katika mji wa Istanbul, ambapo mchezo kati ya Galatasaray na Fernerbahce uliokua unatazamiwa kupigwa Jumapili hii umeahirishwa kutokana na hofu ya kutokea kwa shambulizi.
Polisi ya Uturuki ikipiga doria Machi 20 katika mji wa Istanbul, ambapo mchezo kati ya Galatasaray na Fernerbahce uliokua unatazamiwa kupigwa Jumapili hii umeahirishwa kutokana na hofu ya kutokea kwa shambulizi. AFP

Mchuano ambao ungelizikutanisha klabu mbili kubwa za mjini Istambul Jumapili hii usiku, Galatasaray na Fenerbahçe, umeahirishwa kwa sababu ya hofu ya kutokea kwa shambulizi la "hatari" baada ya lile lililowaua watalii wanne katika mji wa Istanbul Jumamosi hii, serikali ya jimbo imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Mechi ya soka imeahirishwa baada ya tathmini ya kweli ya Idara ya ujasusi" iliyoonyesha hofu ya kutokea kwa shambulizi hatari, serikali ya jimbo imeeleza bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi, katika taarifa iliyotoa saa mbili kabla ya mchezo huo kuanza. mchuano huo ulikua uliingia katika siku ya 26 ya michuano ya ligi kuu ya kitaifa.

Watazamaji ambao walikua wakiingia kwa wingi ili kushuhudia pambanokati ya vlabu hizi hasimu walipokea taarifa ya uamuzi huo kupitia vipaza sauti viliyokua vimewekwa kando ya uwanja na kuombwa kuondoka mara moja eneo hilo, runinga mbalimbali za Uturuki zimearifu.

Askari polisi wengi walitumwa pembezoni mwa uwanja wa Galatasaray, ambapo mchuano kati ya mababe hao wawili ungelianza saa mbili usiku saa za Uturuki, (sawa na 18 jioni saa za kimataifa).

Jumamosi asubuhi, "mshambuliaji wa kujitoa mhanga" alijilipua katika mtaa wa Istiklal, eneo linalotembelewa kila siku na maelfu ya watu, na kuua watu 4, Waisrael watatu na raia 1 kutoka Iran, pamoja na thelathini kujeruhiwa.

Mamlaka ya Uturuki ilisema kuwa mshambuliaji alikuwa raia wa Uturukimwenye uhusiano na kundi la Islamic State (IS).