MAREKANI-SYRIA-IS-MASHAMBULIZi

Syria: namba mbili wa IS auawa na Marekani

Namba mbili wa kundi la Islamic State, Abdel Rahman al-Qadouli, ameuawa katika mashambulizi ya Marekani nchini Syria, Machi 25, 2016.
Namba mbili wa kundi la Islamic State, Abdel Rahman al-Qadouli, ameuawa katika mashambulizi ya Marekani nchini Syria, Machi 25, 2016. AFP/US DEPARTMENT OF STATE

Maafisa kadhaa wa kundi la Islamic State wameuawa wiki hii na mashambulizi ya Marekani nchini Syria, ikiwa ni pamoja na kiongozi namba mbili wa kundi hili, Waziri wa Ulinzi wa marekani ametangaza Ijumaa hii, akizungumza mashambulizi makubwa dhidi ya harakati za kijihadi.

Matangazo ya kibiashara

"Jeshi limewaua magaidi wengi muhimu wiki hii ambapo, tunaamini, Haji Iman, ambaye alikuwa kiongozi wa shirika la Islamic State akihudumia kama Waziri wa Fedha, na ambaye alikuwa pia mkuu wa baadhi ya operesheni za nje," amesema Ashton Carter, huku akiongeza kuwa Marekani imekuwa ikiwaangamiza moja kwa moja viongozi wa kundi la kigaidi, mwandishi wetu katika mji wa Washington, Jean-Louis Pourtet, amearifu.

Haji Iman, pia anaejulikana kama Abdel Rahman al-Qadouli ameuawa na ashambulio lililotekelezwa na vikosi maalum vya Marekani mashariki mwa Syria. Wizara ya Ulinzi ilitoa kitita cha dola milioni 7 kwa ajili ya kukamatwa kwake. Mshirika huyu wa karibu wa Ben Laden alijiunga na kundi la Islamic State, ambapo alikuwa namba 2 na mrithi wa baadaye wa Abu Bakr al-Baghdadi.

Lakini kuangamizwa kwa afisaa huyo na kwa baadhi ya maafisa wengine, kama alivyoeleza Ashton Carter, haina maana, licha ya mafanikio ya kijeshi katika uwanja wa vita, mpaka kundi hili litokomezwe, "Kushambulia viongozi wa juu ni muhimu, lakini haitoshi, amekiri Waziri wa Ulinzi wa Marekani. Kuwaangamiza viongozi wa kundi la IS ni jambo muhimu, lakini watarejelewa katika nafasi zao na tutaendelea kuwalenga. "

Mkuu wa majeshi ya Marekani, jenerali Dunford, kwa upande wake, ametangaza kuwa Pentagon atawasilisha hivi karibuni kwa Rais Barack Obama mapendekezo ya kuimarisha vikosi vya Marekani nchini Iraq, katika maandalizi ya kudhibiti jimbo la Mosul.

Mweka hazina wa Daech

Kumuua Abdul Rahman al-Qadouli ni pia kumuangamiza mfadhili wa kundi la Islamic State. Imamu Haji kwa jina lake maarufu, ni mtu ambaye amekua akirasibu fedha za kundi la IS kama Waziri wa Fedha.