AFGHANISTAN-TALIBAN-SHAMBULIZI

Afghanistan: Taliban yashambulia Bunge kwa roketi bila mafanikio

Jengo ambapo kunafanyika vikao vya Bunge la Afghanistan(kushoto), muda mfupi baada ya shambulizi la kundi la Taliban tarehe 28 Machi, 2016.
Jengo ambapo kunafanyika vikao vya Bunge la Afghanistan(kushoto), muda mfupi baada ya shambulizi la kundi la Taliban tarehe 28 Machi, 2016. REUTERS/Mohammad Ismail

Wapiganaji wa Taliban wamerusha mfululizo wa makombora katika jengo linakofanyia kazi Bunge la Afghanistan, wakati ambapo viongozi wa vyombo vya usalama nchini humo wamekua wakijianda kuzungummza mbele ya Wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Roketi kadhaa zimeanguka katika eneo hilo, na kuharibu madirisha ya majengo, kwa mujibu wa wanasiasa wa Afghanistan. Mamlaka haijasema hasara iliyotokea au majeruhi, na kikao cha bunge kimeendelea bila kukatikizwa.

Kundi la Taliban limedai kuhusika na shambulio hilo, na msemaji wake Zabihullah Mujahid amesema roketi hizo zimesababisha hasara kubwa, ikiwa ni pamoja na watu wengi waliopoteza maisha. Wapiganaji wa kiislamu mara kwa mara wamekua wakitoa idadi isio ua kweli ya watu katika mashambulizi yao.

"Hali hii inatia hofu kuona adui anafikia kulenga majengo ya Bunge, katikati mwa mji, na ni wakati ambapo tumekua tukijadili kuhusu hali ya usalama nchini," mbunge Mohammad Abdou amesema wakati wa kikao cha Bunge kiliyorushwa moja kwa moja. "Hali hii haingetokea," kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Taj Mohammad Jahed, amesema. "Nitaamuru hatua mpya za usalama kwa majengo ya Bunge."

Mashambulizi yalimalizika masaa mawili baadaye, huku washambuliaji saba, ikiwa ni pamoja mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliekua akiendesha gari lililokua limetegwa bomu, wakiuawa na vikosi vya Afghanistan.