SYRIA-IS-PALMYRA-USALAMA

Picha zaonyesha uharibifu mkubwa uliofanywa Palmyra

Mji wa kale wa Palmyra, pamoja na bango linalowaelekeza watalii, Syria, Machi 27, 2016, baada ya serikali kuudhibiti mji huo kutoka mikononi mwa kundi la IS.
Mji wa kale wa Palmyra, pamoja na bango linalowaelekeza watalii, Syria, Machi 27, 2016, baada ya serikali kuudhibiti mji huo kutoka mikononi mwa kundi la IS. STRINGER / AFP

Nchini Syria, vikosi vya serikali vimeurejesha kwenye himaya yao Jumapili hii Machi 27 mji wa kale wa Palmyra, ulioanguka mikononi mwa kundi la Islamic State mwezi Mei 2015.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limesema wanajihadi wameuawa kwa mapigano ya kuuteka mji huo, ikiwa ni hasara kubwa walioipata kwa mapigano hayo pekee tangu kuanza kwa vita nchini Syria. Jeshi la Syria kwa upande wake, limewamepoteza wanajeshi 190.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kurejeshwa kwa mji wa Palmyra kwenye himaya ya jeshi la Syria. "Tuna furaha kwa kweli" baada ya kurejeshwa kwa mji wa Palmyra kwenye himaya ya jeshi la Syria, amesema, huku akipongeza kwamba mamlaka ya Syria inaweza kuwa na uwezo wa "kuhifadhi na kulinda" eneo la kale, ambapo sehemu ya hazina iliharibiwa na wanajihadi.

Hata hivyo picha za Satelite zinaonesha uharibifu mkubwa uliotekelezwa katia mji wa Kihistoria wa Palmyra, muda mfupi baada ya kudhibitiwa na wanajeshi wa Syria.

Mji huo umekuwa ukishikiliwa na wapigani wa Islamic State kwa zaidi ya miezui 10 sasa.

Majengo ya zamani na ya kihistoria yameharibiwa lakini kna baadhi ambayo bado yamesalia.

Rais Bashar Bashir Al Assad amewasifu wanajeshi wake kwa kufanikiwa kuudhibti mji huo na kusisitiza kuwa jeshi lake linadhibiti nchini nzima.