SYRIA-UCHAGUZi-MAPIGANO

Syria: mapigano yaendelea, baada ya uchaguzi

Maafisa wa Idara za huduma za dharura wakimsaidia mwanamke kukimbia mashambulizi ya anga ya jeshi la Syria, kaskazini mwa Aleppo (Haydariya), Aprili 10, 2016.
Maafisa wa Idara za huduma za dharura wakimsaidia mwanamke kukimbia mashambulizi ya anga ya jeshi la Syria, kaskazini mwa Aleppo (Haydariya), Aprili 10, 2016. THAER MOHAMMED / AFP

Serikali ya Syria imeandaa, Jumatano Aprili 13, uchaguzi wa wabunge uliosusiwa na upinzani, na kukosolewa ma nchi za Magharibi, lakini umeungwa mkono na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupiga kura lilifanyika wakati ambapo mkataba wa usitishwaji mapigano, uliotangazwa na Moscow na Washington tarehe 27 Februari, unaonekana kutoheshimishwa.

Mapigano makali yametokea katika jimbo la kaskazini wa Aleppo kati ya jeshi la Syria na washirika wake upande mmoja, na muungano wa waasi, wakiongozwa na Al-Nusra Front, kundi lenye uhusiano na Al Qaeda nchini Syria, upande mwengine. Wakati huo huo, mazungumzo yanaendelea.

■ Mapigano makali katika kijiji cha Al-Eis kati ya Al Nosra na jeshi la serikali

Mapigano hayajasimama kwa siku tano, na yanashuhudiwa hasa kusini mwa mji wa Aleppo, karibu na mji wa Al-Eis, kijiji kidogo muhimu kwa sababu ni kijiji ambacho kinapatikana katika milima iliyo juu ya barabara kuu inayoelekea Damascus na Aleppo.

Jeshi la Syria lilikiweka kwenye himaya yake kijiji cha El-Eis mwezi Januari, kwa msaada wa ndege za kivita za Urusi. Wiki iliyopita, Al-Nusra Front ilikidhibiti baada ykuendesha mashambulizi makali. Tangu wakati huo, vikosi vya serikali na washirika wao wanajaribu kulirejesha kwenye himaya yao, bila mafanikio. Mapigano ni makali na silaha za aina zote zinatumiwa katika mapigano hayo, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita.

■ uchaguzi wafanyika katika vita

Pamoja na vurugu za mapigano, katika maeneo mbalimbali nchini Syria, na licha mkataba wa usitishwaji mapigano uliovunjwa, serikali imeamua kuandaa uchaguzi wa wabunge uliokosolewa na nchi za Magharibi.