SYRIA-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yarindima Syria

Baada ya mashambulizi ya ndege  za kijeshi za Syria Jumamosi jionikatika kata inayoshikiliwa na waasi mashariki mwa Aleppo, kikosi cha Ulinzi wa raia kinaingilia kati ili kutafuta wahanga wa mashambulizi hayo.
Baada ya mashambulizi ya ndege za kijeshi za Syria Jumamosi jionikatika kata inayoshikiliwa na waasi mashariki mwa Aleppo, kikosi cha Ulinzi wa raia kinaingilia kati ili kutafuta wahanga wa mashambulizi hayo. REUTERS/Abdalrhman Ismail

Waasi nchini Syria wameanza kupambana na vikosi vya serikali Jumatatu hii Arili 18, huku wakiushtumu Umoja wa Mataifa kwa kuegemea upande mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya mapya yanatishia mazungumzo ya amani yanayoendelea jijini Geneva nchini Uswisi.

Pande zote mbili zimeendelea kushtumiana kuvunja mkataba wa mwezi Februari kutaka usitishwaji wa mapigano nchini humo ili kuruhusu mazungumzo ya amani.

Waasi wamekuwa wakiwashtumu wanajeshi wa serikali kuwavamia katika mji wa Allepo na hata kutishia kujiondoa katika mazungumzo hayo.

Jumatano juma lilopita serikali ya Syria iliandaa, uchaguzi wa wabunge uliosusiwa na upinzani, na kukosolewa ma nchi za Magharibi, lakini uliungwa mkono na Urusi.

Zoezi la kupiga kura lilifanyika wakati ambapo mkataba wa usitishwaji mapigano, uliotangazwa na Moscow na Washington tarehe 27 Februari, ulionekana kutoheshimishwa.

Wakati huo mapigano makali yalitokea katika jimbo la kaskazini wa Aleppo kati ya jeshi la Syria na washirika wake upande mmoja, na muungano wa waasi, wakiongozwa na Al-Nusra Front, kundi lenye uhusiano na Al Qaeda nchini Syria, upande mwengine, wakati ambapo mazungumzo yalikua yakiendelea.

Machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Syria yamesababisha maefu ya raia kuuawa na mamia kwa maelfu kukimbilia nchi jirani.