IRAQ-MASHAMBULIZI

Watu 33 wauawa kusini mwa Iraq

Baghdad imekumbwa Jumatatu, Januari 11, 2016 na mashambulizi ambapo kundi la Islamic Sate lilidai kutekeleza shumbulizi moja.
Baghdad imekumbwa Jumatatu, Januari 11, 2016 na mashambulizi ambapo kundi la Islamic Sate lilidai kutekeleza shumbulizi moja. REUTERS/Ahmed Saad

Watu wasiopungua 33 wameuawa na wengine hamsini wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili yamabomu yaliotegwa ndani ya magari katika mji wa Samawah kusini mwa Iraq, kwa mujibu wa kiongozi wa matabibu na viongozi wa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Milipuko miwili, ambayo haijadaiwa na kundi lolote, imepiga katika eneo la katikati ya mji, wakati ambapo mikoa ya kusini mwa nchi mara nyingi inatengwa na mashambulizi kama hayo.

"Hospitali zimepokea watu 33 waliopoteza maisha," mtabibu mmoja wa hospitali ya mkoa wa Mouthanna ameliambia shirika la habari la AFP. Mmoja wa viongozi wa shughuli za mkoa amethibitisha idadi hiyo.

"Gari la kwanza lililipuka saa sita mchana karibu na kituo cha mabasi katikati mwa mji, ikifuatiwa dakika tano baadaye na mlipuko wa gari la pili kwenye umbali wa mita 400 na eneo kulikotokea mlipuko wa kwanza.

Samawah (klilomita 230 kusini mwa Baghdad) ni mji mkuu wa jimbo la Muthanna unaopakana na Saudi Arabia, na unapatikana katikati mwa mkoa unaokaliwa na wakazi wengi hasa kutoka jamii ya Mashia.

Jumamosi, bomu lilitegwa ndani ya gari ndogo karibu na mji wa Baghdad, likiwalenga mahujaji wa Kishia. Shambulizi ambalo lilisababisha vifo vya watu 23 na kundi la kijihadi la Islamic State (IS) limekiri kutekeleza shambulizi hilo.

Kundi la Islamic State bado linadhibiti maeneo makubwa katika ardhi ya Iraq magharibi na kaskazini mwa Baghdad, lakini limeendelea kupoteza nguvu katika uwanja wa vita dhidi ya vikosi vya Iraq, vinavyoungwa mkono na muungao wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Hayo yakijiri maelfu ya waandamanaji wamekusanyika Jumapili hii katika Eneo linalolindwa vikali baada ya siku moja kuyadgibiti majengo ya Bunge kwa muda wa saa kadhaa, wakati ambapo Waziri Mkuu Haider al-Abadi alitoa wito wa kuwaadhibu watu wanaohusika na machafuko.

Jumamosi, waandamanaji walivamia eneo hilo ambpo kunapatikana taasisi mbalimbali za nchi hiyo na balozi za kigeni, ili kulikemea Bunge kwa kutochukua hatua zinazofaa kwa maslahi ya taifa na wananchi wake pamoja na kudai serikali mpya yenye uwezo wa kutekeleza mageuzi ya kupambana na rushwa.