SYRIA-UN-MAPIGANO

Moscow kuwa na matumaini ya kufikiwa kwa mkataba Aleppo

Mtu akitembea katika mtaa wa Aleppo ulioharibiwa na mashambulizi, Mei 2, 2016.
Mtu akitembea katika mtaa wa Aleppo ulioharibiwa na mashambulizi, Mei 2, 2016. AFP

Moscow imesema Jumanne hii kuwa ina matumaini ya kufikiwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano "katika masaa yajayo" katika jimbo la Aleppo, mji mkubwa uliyogawanyika kaskazini mwa Syria, ambako mapigano mapya na mashambulizi yamewaua watu 18, na kituo cha matibabu kinaaminika kuwa kimeshambuliwa katika mapigano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, Ufaransa na Uingereza wameomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuhusu jimbo la Aleppo, Mabalozi wa nchi hizi wamesema Jumanne hii.

Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Matthew Rycrofti, ambaye amebaini kwamba Allepo inateketea kwa moto amesema ni faili ambayo inatakiwa ipewe "kipaumbele zaidi".

Kwa mujibu wa mpiga picha anayefanya kazi kwa shirika la habari la AFP, hii ni siku ya kutisha imeshuhudiwa katika eneo linalodhibitiwa na utawala wa Bashar al-Assad tangu kuanza kwa machafuko Aprili 22 katika mji wa pili wa Syria, ambapo zaidi ya watu 270 wameuawa katika muda wa siku 12.

Kuengezeka kwa machafuko haya kumesababisha kuvunjika kwa mkataba wa usitishwaji mapigano ulianza kutekelezwa Februari 27 chini ya shinikizo la Urusi, mshirika wa serikali, na Marekani inaunaga mkono upinzani.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura, ambaye ameonya kuhusu machafuko hayo, amefanya ziara mjini Moscow Jumanne hii kukutana na Waziri Urusi mwenye dhamana ya Mambo ya nje, Sergei Lavrov.

"Tunapaswa kuhakikisha kwamba usitishwaji wa mapigano unatekelezwa upya" waziri wa mambo ya nje wa Urusi amemwambia Staffan de Mistura.

Hali isiyovumilika

Lavrov aamesema ana matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano "katika masaa yajayo" juu ya mapigano katika jimbo la Aleppo. "Natumaini kwamba, mara, pengine hata katika saa chache zijazo, uamuzi huo utatangazwa," Lavrov amesema.

Bw de Mistura, ambaye alifanya mazungumzo Jumatatu hii na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, anataka Urusi na Marekani wajaribu kuzishawishi pande zinazokinzana kuafikiana upya mkataba wa usitishwaji wa mapigano.

Kerry, hata hivyo, alisema Jumatatu kuwa mgogoro sasa "umeshindwa kudhibitiwa. "

Wakati huo huo, Ujerumani imetangaza mazungumzo Jumatano mjini Berlin na Bw de Mistura, mratibu wa upinzani nchini Syria Riad Hijab na waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault.

"Mazungumzo haya yatalenga swali la jinsi ya kujenga mazingira kwa ajili muendelezo wa mazungumzo ya amani mjini Geneva, ili kupunguza vurugu na kuboresha hali ya kibinadamu nchini Syria," Wizara wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema.

"Kinachotokea katika jimbo la Aleppo hakivumiliki (...) tunapaswa kufanya kila liwezekanalo ili mapigano yakome (...)," Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema.

Katika uwanja wa mapigano, waasi wameendesha mashambulizi makubwa kwa dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na jeshi la serikali ya Aleppo, ambapo watu wasiopungua 16 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, shirika la habari nchini Syria la SANA limearifu.

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), kwa upande wake linatoa idadi ya watu 19 waliouawa na wengine 80 kujeruhiwa, baadhi wakiwa wamejeruhiwa vibaya.