ISRAEL-PALESTINA-SHERIA

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji apewa kifungo cha juu Israel

Hussein (kushoto), baba wa kijana wa Kipalestina wa miaka 16, Mohammed Abu Khdeir, aliyeuawa mwezi Julai 2014, na Ahmad al-Tibi, Mbunge Mwarabu mwenye asili ya Israel, Jerusalem Aprili 19, 2016.
Hussein (kushoto), baba wa kijana wa Kipalestina wa miaka 16, Mohammed Abu Khdeir, aliyeuawa mwezi Julai 2014, na Ahmad al-Tibi, Mbunge Mwarabu mwenye asili ya Israel, Jerusalem Aprili 19, 2016. AFP

Mahakama ya Jerusalem imemuhukumu Jumanne hii kifungo cha maisha jela, hukumu kubwa iwezekanayo, mtuhumiwa mkuu, raia wa Israel, katika mauaji ya raia mmoja wa Palestina aliyechomwa moto akiwa hai mwaka 2014, uhalifu ambao ulichangia kupanda kwa vurugu na kusababisha vita katika Ukanda wa Gaza.

Matangazo ya kibiashara

Yosef Haim Ben David, Myahudi, mwenye umri wa miaka 31, alikuwa alishitakiwa kuwa mratibu na mhusika mkuu katika utekaji nyara na mauaji ya kijana wa Kipalestina, mwenye umri wa miaka16, Mohammed Abu Khdeir, Julai 2, 2014 katika mji wa Jerusalem Mashariki, sehemu ya Palestina inayodhibitiwa na Israel.

Washirika wake wawili, Wayahudi wa Israel, wenye umri wa miaka 16, mwezi Julai 2014, walihukumiwa, mmoja kifungo cha maisha jela na mwengine kifungo cha miaka 21 jela Februari 4 na mahakama hiyo. Majina yao yamewekwa siri kwa sababu walikuwa watoto wakati tukio hilo.

Uhalifu, unaochochewa kwa sababu za ulipizaji kisasi, ulmeshuhudiwa kwa kiasi kikubwa kwa raia wa Palestina. Wakati mahakama ilipotangaza uamuzi wake, familia ya Mohammed Abu Khdeir ilipumua baada ya kuwa na hasira kwa kipindi cha miaka miwili, huku ikitoa matusi dhidi ya Ben David licha ya mtuhumiwa huyu kuonyesha masikitiko yake baadaye na kuomba aweze kunyongwa.

Uamuzi wa mahakam umetolewawakati ambapo machafuko yameendelea kushika kasi kati ya Waisrael na Wapalestina, mashambulizi ambayo yamegharimu maisha ya watu 200 tangu Oktoba 1, 2015.

Kifungo cha maisha ni adhabu ya juu kabisa ambayo mahakama ingeweza kuchukua. Mbali na uhalifu maalum kama vile uhalifu wa kivita au uhaini, adhabu ya kifo ilifutwa tangu mwaka 1954.

Mahakama pia imemuamuru kulipa Shekel 150,000 (sawa na Euro 34,400) kwa kwa familia ya Mohammed Abu Khdeir na Shekel 20,000 (sawa na Euro 4500) kwa familia ya mtoto aliyejaribu kuteka nyara.