SYRIA-MKATABA

Mkataba kati ya Marekani na Urusi kwa kusitisha mapigano Aleppo

Vikosi vya usalama vya Syria vikiwaokoa wafanyakazi wa hopitali ya Muhafaza Aleppo, baada ya waasi kuendesha mashambulizii, Mei 3 2016.
Vikosi vya usalama vya Syria vikiwaokoa wafanyakazi wa hopitali ya Muhafaza Aleppo, baada ya waasi kuendesha mashambulizii, Mei 3 2016. GEORGE OURFALIAN / AFP

Nchini Syria, mapigano na mashambulizi ya anga yameendelea, lakini vita vingine vya kidiplomasia kwa sasa, vimeanza kushuhudiwa kwa kusitisha uhasama katika jimbo la Aleppo.

Matangazo ya kibiashara

Urusi na Marekani wanataka kurejesha haraka iwezekanavyo mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika mji huo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha usiku wa Jumatano hii makubaliano kati ya Washington na Moscow juu ya ujenzi wa mji wa Aleppo na usitishwaji wa mapigano.

Ni kwa taarifa fupi ambapo wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha makubaliano hayo. Mkataba huu "unaanza kutekelezwa leo saa 6:01 usiku wa manane" (sasa za Syria) "katika jimbo la Aleppo, ikiwa ni pamoja na katika mji wa Aleppo," imesema taarifa hiyo. "Tumeshuhudia kwamba machafuko yamepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo hayo, ingawa kuna taarifa za kuendelea kwa mapigano katika baadhi ya maeneo," Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani, imesema katika taarifa yake.

Moscow itaongeza mara mbili jitihada zake za kumshawishi rais wa Syria Bashar al-Assad kwa kuzingatia mkataba huu. Washington, kwa upande wake, itafanya hivyo kwa upinzani. Mgawanyo huu wa majukumu kati ya nchi hizi mbili tayari ulipelekea kuhitimisha mkataba wa ndani katika mkoa wa Latakia na Damascus, ni mpango huu unapaswa kufuatwaili kupunguza ukali wa mapigano na mashambulizi katika jimbo la Aleppo.

Imekua ni siku kadhaa, karibu wiki, ambapo Urusi na Marekani walikuwa wakiwasiliana moja kwa moja kufikia usitishwaji wa uhasama na hasa zaidi, kupanua mikataba ya kurejesha utulivu iliyoafikiwa siku kumi zilizopia, kwa mkoa wa Damascus.