MAREKANI-IS-USALAMA

Jeshi la Marekani ladai kumuua kiongozi mkuu wa IS

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wakisem akuwa wataendelea na harakati yao..
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wakisem akuwa wataendelea na harakati yao.. Reuters

Jeshi la Marekani limetangaza kwamba limemuua katika shambulio la anga mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la kijihadi la Islamic State, Abu Waheeb.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imesema kundi la Islamic ste imepata pigo kubwa kufuatia kifo hicho cha mmoja a wakuu wa kundi hilo katika mkoa wa Anbar, nchini Iraq.

Abu Waheeb alikamatwa na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na kuhukumiwa kifo lakini alifaulu kutoroka jela mwaka 2012.

Wahib alizaliwa ambaye alizaliwa 1986 alikuwa mwanafunzi wa zamani wa sayansi ya kompyuta na alielezwa na mitandao mbali mbali inayofuatilia shughuli za kundi la Islamic State kama mtu ambaye alikua mashuhuri katika kundi hilo.

Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema Abu Waheeb, aliuawa pamoja na watu wengine watatu baada ya gari lao kushambuliwa na ndege ya Marekani katika eneo la Rutba.