IRAQ-MASHAMBULIZI

Iraq: mashambulizi ya IS yaua watu 94 karibu na soko Baghdad

Bomu lilitegwa ndani ya gari ndogo na kulipuka katika mtaa unaokaliwa na Mashia wa Sadr City  mjini Baghdad, wakati wa soko Jumatano hii Mei 11, 2016.
Bomu lilitegwa ndani ya gari ndogo na kulipuka katika mtaa unaokaliwa na Mashia wa Sadr City mjini Baghdad, wakati wa soko Jumatano hii Mei 11, 2016. REUTERS/Wissm al-Okili

Watu wasiopungua 94 wameuawa Jumatano hii katika mashambulizi matatu ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika mji wa Baghdad, ambapo shambulio moja limelenga soko moja lililokua limejaa watu wengi.

Matangazo ya kibiashara

Mji mkuu wa Iraq umekumbwa Jumatano hii mashambulizi mabaya kabisa yaliyosababisha vifo vya watu wengi.

Mashambulizi matatu, ambayo pia yamewajeruhi watu 150, yamedaiwa kutekelezwa katikataarifa zilizorushwa hewani na kundi la wanajihadi wa dhehebu la Sunni, Islamic State (IS) ambalo limethibitisha kwamba washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga ndio wametekeleza shambulio hilo.

Mashambulizi haya yanatokea katika mazingira ya mgogoro wa kisiasa nchini humo, ambayo kwa mujibu wa wataalamu yanaweza kudhoofisha mapambano ya vikosi vya Iraq dhidi ya wapiganaji wa kijihadi.

Shambulizi baya kabisa lilitokea saa moja kabla ya mashambulizi mengine katika eneo la soko la mtaa unakaliwa na Mashia wa Sadr City, kaskazini mwa mji wa Baghdad. Kwa uchache watu 64 wamefariki na 82 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa madaktari na vyombo vya usalama.

"Watu na wauzaji hapa ni raia wasio na hatia," amesema shahidi Abou Ali ambaye alionyesha hasira yake.

- "Wanasiasa wanapaswa kuondoka" -

Masaa machache baadaye, mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari yalitokea katika maeneo mengine mawali ya mji wa Baghdad, kwa mujibu wa polisi.

Mta wa Kazimiyah, unaokaliwa na Mashia ulio chini ya ulinzi mkali kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bghdad, shambulizi limewaua kwa uchache watu 17, kwa mujibu wa vyanzo vya hospitali. askari polisi wengi ni miongoni mwa wahanga.

Katika kitongoji kinachokaliwa na watu kutoka madhehebu ya Masunni na Mashia cha Jamea, magharibi mwa mji wa Baghdad, watu 13 wameuawa katika mlipuko mwengine, kwa mujibu afisa wa serikali.