IS yatoa video ikiwauawa raia Iraq
Imechapishwa:
Kundi la kigaidi la Islamic State limetoa mkanda wa Video, likiwauwa wanaume watano mbele ya kundi la watu.
Video hiyo ya dakika 12 imekuwa ikionekana katika mitandao ya kijamii, huku watu wakionekana wakiulizwa maswali.
Mkanda huo pia unaonesha kuharibiwa kwa mji wa Mosul kutokana na mashambulizi yaliyotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.
Watoto kadhaa waliopoteza maisha pia wanaonekana katika mkanda huo.
Kitu kingine kinachoonekana katika mkanda huo ni pamoja na watu kuhojiwa kuhusu mauaji yanayotekelezwa na kundi hilo linaloendelea kuisumbua dunia.
Wakati huo huo kundi hilo la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi la kigaidi mapema mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 94.