SYRIA-HEZBOLLAH

Syria: Amiri jeshi mkuu wa Hezbollah auawa

Kiongozi mkuu wa Hezbollah Mustafa Badreddine.
Kiongozi mkuu wa Hezbollah Mustafa Badreddine. AFP

Hezbollah imetoa taarifa ikisema kuwa mlipuko mkubwa umetokea katika kambi ya wapiganaji wa Hezbollah karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus, kusini mwa mji mkuu, na kuua Mustafa Badreddine na kuwajeruhi watu wengine kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Hezbollah imetangaza Ijumaa hii kifo cha kiongozi wake wa kijeshi nchini Syria Mustafa Badreddine, mmoja wa wajumbe watano wa Hezbollah wanatuhumiwa mauaji ya Rafik Hariri, aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon.

"Alisema miezi michache iliyopita," Sintorudi kutoka Syria, hadi pale umauti utanikuta au nirudi nimeshikilia bendera ya ushindi. "hii ni kauli ya amri jeshi mkuu wa Hezbollah, Mustafa Badreddine. Leo amrudi akiwa shahidi, " Hezbollah imesema taarifa iliyorushwa kwenye runinga ya Al-Manar.

Hezbollah imesema kwamba uchunguzi unaendelea ili kujua sababu za mlipuko huo.

"Tutaendelea na uchunguzi kujua sababu za mlipuko na kujua kama ni kutokana na shambulizi la anga, kombora au kitu kingine," Hezbollah imesema bila kunyooshea kidole upande wowote.

Hezbollah ni adui mkubwa wa Israel na iliwekwa katika orodha ya "makundi ya kigaidi" na Marekani.

Kundi hili la Kishia kutoka Libanon limekua likiituhumu Israel kwa mauaji ya maafisa wake, lakini halijaeleza iwapo Israel inahusika katika kifo cha Badreddine.