Mashambulizi mawili ya IS yasababisha vifo Yemen
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kundi la Islamic State limetekeleza Jumapili hii Mei 15 mashambulizi mawili nchini Yemen. Mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yamesababisha vifo vya watu 37 miongoni mwa vikosi vya usalama katika mkoa wa Hadramout kusini mwa nchi hiyo.
Katika suala la makundi ya wanajihadi, eneo la kusini mwa Yemen lmekua mpaka sehemu ya mawindo kwa kundi la AQPA, al-Qaeda katika Peninsula ya Arabia, lakini kundi la Islamic State linaonekana kukuta mizizi katika jimbo hilo.
Kupitia mashambulizi haya mawili, ni ujumbe uliyotumwa na kundi la Islamic State. Ujumbe wa kwanza unahusu vikosi vya usalama vya Yemen. Shambulio la kujitoa mhanga la Jumapili hii kwanza limelenga mkutano wa polisi. Wahanga walikuwa vijana walioajiriwa katika polisi. Kisha shambulio la pili pia limelenga jengo la polisi.
Jenerali Mubarak al-Oubthani, mkuu wa polisi katika mkoa wa Hadramout, aliponea chupuchupu katika mashambulizi hayo. Inaarifiwa kuwa alikuwepo wakati wa mashambulizi yote mawili, lakini inasemekana kuwa amejeruhiwa kidogo.
Ujumbe mwengine wa wanajihadi wa kundi la Islamic State, pengine umetumwa kwa mahasimu wao AQPA. Jimbo la Hadramout ni ngome ya wapiganaji wa Al-Qaida katika Peninsula ya Arabia (AQPA) kwa miaka ishirini.
Katika wiki za hvi karibuni kundi la Islamic State lilionekana kuwa na nguvu zaidi. Kundi hili la kigaidi linatoa zaidi hisia ya kurejelea kuni la Al-Qaeda katika jimbo hili la kusini mwa Yemen.
Nchi inayokumbwa na vita kati ya jeshi na waasi wa Kishia wa Houthi inakabiliwa na mashambulizi ya kijihadi. Makundi ya IS na Al-Qaeda yanachukulia hali ya machafuko inayojiri nchini humo kwa kuimarisha harakati zao kusini mwa Yemen.