IRAQ-MASHAMBULIZI

Iraq: Baghdad yakumbwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya

Shambulizi baya kabisa, shambulizi la kujitolea muhanga kwa bomu lililotegwa ndani ya gari, limelitikisa eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City kaskazini mwa Baghdad, na kuua watu 21.
Shambulizi baya kabisa, shambulizi la kujitolea muhanga kwa bomu lililotegwa ndani ya gari, limelitikisa eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City kaskazini mwa Baghdad, na kuua watu 21. REUTERS/Khalid al Mousily

Watu wasiopungua 39 wameuawa Jumanne hii katika mfululizo wa mashambulizi mapya yaliyotokea katika mji wa Baghdad. Hii ikiwa ni idadi ya muda iliyotolewa na serikali ya Iraq. Mji wa Baghdad unashuhudia wiki ya pili ya mfululizo wa machafuko.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano iliyopita, eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City lilikumbwa na mashambulizi.

Kwa wiki moja sasa, mashambulizi yamekua yakiendelea katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Mfumo unaotumiwa katika mashambulizi hayo ni mmoja: Mabomu yanayotegwa ndani ya magari katika mitaa ya Baghdad au mshambuliaji wa kujitoa mhanga analipua mkanda wenye kulipuka katikati ya soko, na hivyo kusababisha watu wengi kupoteza maisha.

Jumanne hii, maeneo matatu nchini Iraq yamekumbwa na mashambulizi haya, ikiwa ni pamoja na kitongoji kikubwakinachokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia cha Sadr City. Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi haya, lakini kundi la Islamic State (IS) lilikiri kuhusika na mashambulizi ya wiki iliyopita dhidi ya Mashia, wanaochukuliwa na wanajihadi kama maadaui wa kwanza.

Wapiganaji hawa wa "Khalifa" ambao wanasakamawa kwa mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa na vikosi vya Iraq waonekana kuwa wamebadilishwa mkakati.

Mbali na mapigano katika uwanja wa vitai kunashuhudiwa kwa sasa ongezeko la mashambulizi ya kujitoa muhanga.

Tangu kuanzishwa kwake kundi la Islamic State limefika mara kadhaa karibu na mji mkuu wa Iraq. Lakini wapiganaji wake hawajawahi kuudhibiti mji wa Baghdad. Njia pekee ambayo wamebaki nayo kwa kufikia mji mkuu, ni mashambulizi ambayo mara kwa mara yamekua yakigharimu maisha ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Iraq.