SYRIA-AMANi

Jitihada mpya za kidiplomasia kwa kuokoa mazungumzo ya amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov (kulia) wamewasili Vienna Jumatatu, Mei 16, kwa mkutano wao Jumanne hii.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov (kulia) wamewasili Vienna Jumatatu, Mei 16, kwa mkutano wao Jumanne hii. REUTERS/Leonhard Foeger

Nchi zenye nguvu duniani zitajaribu kuzindua Jumanne hii mjini Vienna mazungumzo juu ya amani nchini Syria ambayo hivi karibuni yaliingia hatarini, kutokana na ukiukwaji wa makubaliano ya usitishwaji wa mapigano na kuzuia wa misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la kimataifa linalounga mkono mchakato wa amani wa Syria (GISS) linaloongozwa na Marekani na Urusi, linakutana saa 9:00 asubuhi (sawa na saa 700 saa za kimataifa) katika mji mkuu wa Austria, Vienna.

Washington itaweka kwenye meza malengo matatu yaliyoafikiwa kwa kusitisha vita hivi hatari, "kuimarisha makubaliano ya usitishwaji wa uhasama (...) kuhakikishamisaada ya kibinadamu inawafikia walengwa nchini kote na kuongeza kasi kwa taasisi ya mpito ya kisiasa," kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Mkataba wa mazungumzo unaweka wazi kwamba hadi Agosti 1 taasisi ya mpito ya kisiasa iwe imekwisha wekwa chini ya azimio la Umoja wa Mataifa, lakini tarehe hii ya mwisho inaonekana kutoweza kuheshimishwa.

"Lengo kwa mwezi wa Agosti ni kuwa na taasisi katika mfumo wa makubaliano kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa, " afisa mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema mbele ya waandishi wa habari mjini Vienna.

Hatima ya Rais Bashar al-Assad bado haijatatuliwa na suala hili ndio linazua hali ya kutoelewana kati ya mataifa yenye nguvu duniani na kikanda yanayounga mkono mchakato wa amani nchini Syria (GISS), kundi la nchi 17 na mashirika matatu ya kimataifa - ikiwa ni pamoja na Marekani, Urusi, Saudi Arabia, Iran na Umoja wa Ulaya.

Licha ya kusaidia jitihada za kidiplomasia za GISS, Moscow na Tehran wamekua wakitoa msaada wa kijeshi kwa utawala wa Syria katika uwanja wa vita.

- Mapigano karibu na Damascus -

Wakati ambapo juhudi za kurejesha amani nchini Syri zikiendelea, mapigano yamekua yakirindima katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Hata hivyo makubaliano ya usitishwaji wa mapigano yaliyoafikiwa mwishoni mwa mwezi Februari chini ya shinikizo la Urusi na Marekani yamevunjwa.

Mapigano makali tangu siku ishirini kati ya makundi hasimu ya Kiislam kwa lengo la kudhibiti ngome ya waasi karibu na jimbo la Damascus yamewaua zaidi ya 300, sirika lisilo la kiserikali liliarifu Jumapili, mwishoni mwa juma lililopita.