YEMEN-SERIKALI YA UMOJA

Serikali ya umoja uliopendekezwa na waasi yafutiliwa mbali

Vikosi vinavyounga mono serikali wakati wa mapigano na wanamgambo wa Kishia katika mji wa Al Karsh Yemen, Mei 13, 2016.
Vikosi vinavyounga mono serikali wakati wa mapigano na wanamgambo wa Kishia katika mji wa Al Karsh Yemen, Mei 13, 2016. AFP

Waziri Mkuu wa Yemn, Ahmed bin Dagher, amekataa Jumatano hii mapendekezo ya serikali ya umojayaliyotolewa na waasi, ambao anawashtumu kuhatarisha umoja na uchumi wa nchi. Yemen inaendelea kukumbwa na vita kwa zaidi ya mwaka sasa.

Matangazo ya kibiashara

Bw Bin Dagher, ambaye amezungumza na waandishi wa habari mjini Riyadh ambako anaishi uhamishoni, amesema kuwa waasi wa Kishia wa Houthi wanapaswa kurejesha silaha na kuondoka katika maeneo wanayoshikilia, ikiwa ni pamoja mji mkuu Sanaa,tangu kushindwa mapinduzi dhidi ya serikali mwaka 2014, kwa mujibu wa azimio 2216 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

"Kuondoka kwa (waasi) katika taasisi za serikali ni suala lisiokua na masharti" na serikali ndio pekee "kikatiba" inaruhusiwa kumiliki silaha za kivita nchini, Bin Dagher ameonya wakati ambapo mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi yanapiga hatua nchini Kuwait.

Wakati wa mazungumzo, yaliyoanzishwa Aprili 21 chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, waasi wanashirikiana na wafuasi wa rais wa zamani aliyeondolewa madarakani Ali Abdullah Saleh walipendekeza kuwepo na serikali ya mpito kabla ya utekelezaji wa azimio 2216.

Waziri Mkuu amewakemea "wale ambao wanataka serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kukabidhi silaha yao," akisisitiza kuwa Yemen, ambayo inaadhimisha Jumapili miaka 26 ya muungano wake, iko mbele ya "chaguo la kihistoria" kuhifadhi "umoja"wake au hatari ya "kugawanyika".