IRAQ-IS

Iraq yaanzisha operesheni dhidi ya IS Falluja

Tarehe 21 Mei 2016, jeshi la Iraq karibu na mji wa Fallujah, likiandaa shambulio la kuichukua ngome hiyo kutoka mikonomwa IS.
Tarehe 21 Mei 2016, jeshi la Iraq karibu na mji wa Fallujah, likiandaa shambulio la kuichukua ngome hiyo kutoka mikonomwa IS. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi ametangaza kuanza operesheni ya kijeshi kuuchukua mji wa Falluja kutoka kwa kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limetoa wito kwa raia wanaoishi katika mji huo kuanza kuondoka kabla ya kuanza kwa mashambulizi hayo.

Hata hivyo, wakazi ambao hawataweza kuondoka wameshauriwa kusimika bendera nyeupe juu ya nyumba zao ili kutambuliwa na jeshi.

Mji wa Falluja ulikuwa wa kwanza, kudhibitiwa na kundi la Islamic State mwaka 2014 na ndio mji unaosalia mikononi mwa magaidi.