SYRIA-IS-MASHAMBULIZI

IS yashambuliwa Syria

Mpiganaji wa vikosi vya Wakurdi, akipiga kambi kilomita hamsini na mji wa Raqqa, Oktoba 2015.
Mpiganaji wa vikosi vya Wakurdi, akipiga kambi kilomita hamsini na mji wa Raqqa, Oktoba 2015. AFP PHOTO / DELIL SOULEIMAN

Kundi la wapiganaji linaloungwa mkono na Marekai limewashambulia wapiganaji wa Islamic State katika mji wao mkuu wa Raqqa nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la Syrian Democratic Forces linaloshirikiana na wapiganaji wa Kikurdi wameanza mashambulizi hayo baada ya kufanikiwa kudhibitiwa maeneo mengi ya Kaskazni na Mashariki mwa nchi hiyo.

Hadi sasa mwendelezo wa operesheni hiyo haijafahamika.

Serikali ya Syria imekuwa ikisema wapiganaji hao ni wachache sana na hawawezi kupambana na Isamic State.