IRAQ-SYRIA-IS

Majeshi yanayopambana dhidi ya IS yasonga mbele Syria na Iraq

Operesheni ya vikosi vya Iraq dhidi ya kundi la Islamic State, Mei 26, 2016 karibu na mji wa Fallujah, Iraq.
Operesheni ya vikosi vya Iraq dhidi ya kundi la Islamic State, Mei 26, 2016 karibu na mji wa Fallujah, Iraq. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani nchini Iraq na Syria vimesonga mbele Alhamisi katika mashambulizi yao dhidi ya kundi la Islamic State (IS), wachambuzi wanaeleza, hata hivyo, kwamba vita hivyo vinaweza kuchukua muda mrefu.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Syria ambayo imeathirika zaidi na vita kwa miaka mitano, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Staffan de Mistura, ameonya kuwa raia wengi waliokwama katika mapigano "wanaweza kufaa kwa njaa" kama misaada ya kibinadamu haitowafikia haraka katika maeneo yao kadhaa.

Zaidi ya watu 280,000 wameuawa katika vita nchini Syria, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), wakati ambapo mamilioni wamelazimika kuyahama makazi yao.

Katika vita hivi vinavyoshuhudiwa katika maeneo mengi nchini Iraq na Syria, mapigano yanaonekana kuwa kukita mizizi dhidi ya kundi la IS katika mkoa wa Raqa (kaskazini-mashariki) ambapo yanaendelea mashambulizi makali yaliyoanzishwa Jumanne iki hii na muungano wa majeshi ya Kiarabu kwa ushirikiano na Wakurdi kwa msaada wa mashambulizi wa muungano kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Muungano wa vikosi vya FDS vinataka kulitimua kundi la IS kaskazini mwa mkoa wa Raqa, unaodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na kundi hilo.

FDS imedai katika taarifa yake kwamba "ilividhibiti vijiji vitano pamoja ikiwa ni pamoja na Fatsa, Namroudiya, Wasta na mashamba manne."

Kwa mujibu wa OSDH, FDS inaendelea na mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la IS karibu na mji wa Ain Issa, wakati muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekaniukiendelea na mashambulizi yasiyo koma.