BAHRAIN-MASHIA

Mashia sita wahukumiwa kifungo cha maisha

Hamed ben Issa al-Khalifa, Mfalme wa Bahrain picha ilipigwa mwaka 2013 Beijing.
Hamed ben Issa al-Khalifa, Mfalme wa Bahrain picha ilipigwa mwaka 2013 Beijing. AFP PHOTO / POOL / Feng Li

Mahakama Kuu ya Rufaa nchini Bahrain imetangaza hukumu dhidi ya mashia watatu kwa kuhusika na kosa la mauaji ya askari polisi watatu katika nchi ya Ghuba, inayokabiliwa namachafuko ya hapa na pale tangu mwaka 2011, chanzo mahakama kimesema.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu ya kifungo cha maisha pia imetangazwa kwa watuhumiwa sita wengine kati ya sabaMtuhumiwa wa saba hakukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa mwezi Februari 2015, chanzo hicho kimesema.

Washtakiwa kumi walikutwa na hatia ya kutekeleza mashambulizi Machi 3, 2014 katika kijiji kinachokaliwa na Mashia, ambapo askari polisi watatu, akiwemo afisa kutoka Emirati, waliuawa.

hili ni shambulizi baya kabisa tangu kulipuka, mwezi Machi 2011, kwa ghasia zilizozushwa na maandamano ya Mashia walio wengi dhidi ya jamii ya Masuni wanaotawala nchini humo, ambao pia ni mshirika wa Washington.

Pia ni mara ya kwanza askari polisi kutoka nchi nyingine ya Ghuba kuuawa nchini Bahrain, ambapo wanajeshi na askari polisi wa nchi jirani walitumwa miaka minne ili kusaidia utawala wa kifalmewa Kisunni dhidi ya uasi wa Kishia.

Siku ya Jumatatu, kiongozi wa upinzani kutoka jamii ya Mashia, Sheikh Ali Salman, alihukumiwa baada ya kukata rufaa kwa miaka tisa jela kwa kuhusika na uchochezi wa maandamano na njama dhidi ya serikali, uamuzi mgumu zaidi kuliko miaka 4 gerezani aliyohukumiwa katika mahakama ya mwanzo.