IRAQ-FALLUJAH-IS

Vikosi vya Iraq vyaendelea na mashambulizi Fallujah

Operesheni ya vikosi vya Iraq dhidi ya kundi la Islamic State, Mei 26, 2016 karibu na mji wa Fallujah, Iraq.
Operesheni ya vikosi vya Iraq dhidi ya kundi la Islamic State, Mei 26, 2016 karibu na mji wa Fallujah, Iraq. AHMAD AL-RUBAYE / AFP

Vikosi maalum vya Iraq vimeimarisha mashambulizi yake katika mji wa Fallujah kuwaondoa wapigaji wa Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya iraq vimekuwa vikisonga mbele kuanzia jana Jumatatu katika harakati za kuwaondoa kabisa wapiganaji hao wa Islamic State waliochukua mji huo mwaka 2014.

Serikali ya Iarq inasema, vikosi vyake vikisaidiwa na vile vya Kimataifa vilianza mashambulizi hayo kwa kutumia ndege za kivita na vimepiga hatua kubwa.

Hata hivyo, kumeripotiwa kuwepo kwa visa vya kujibiwa kwa mashambulizi ya kundi la Islamic State katika ngome hii ambayo wamekuwa wakiidhibiti wa muda mrefu sasa.

Hadi sasa zaidi ya wanajeshi 10 wa Iraq wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika harakati za kuukomboa mji huu.

Maelu ya watu wamefanikiwa kuyakimbia makwao lakii kuna hofu kuwa zaidi ya elfu 50 wameshindw akuondoka kwa sbabau ya kuendelea kwa makabiliano hayo.